CHADEMA yaifunika CUF

Upanga Mkali

Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
96
Reaction score
83
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]WAKATI wananchi wakishangaa jinsi vyama vya upinzani kupitia kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vilivyopata mafanikio kwa kiasi fulani dhidi ya chama tawala, CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliyokamilika hivi karibuni nchini kote, upo mshangao mwingine kuhusu namna Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilivyo kipiku Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi huo.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
CUF, moja ya chama kikuu cha upinzani nchini ambacho kiliongoza vyama vyote vya upinzani kwa kupata mafanikio makubwa kisiasa katika uchaguzi kama huo uliyofanyika mwaka 2009, tofauti na matarajio ya wafuasi wake, mwaka huu kimefanya vibaya ikilinganishwa na chama kingine kikuu cha upinzani, Chadema.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji (TAMISEMI), Khalist Luanda, ukiacha ushindi wa jumla ambao ulinyakuliwa na chama tawala, CCM, chama kilichofuatia kwa kupata mafanikio katika uchaguzi huo, ni Chadema.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi, wakati CCM imevuna ushindi wa jumla wa Mitaa na Vijiji 9,406, vyama vya upinzani ambavyo wakati mwingine hufahamika kama
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT], vimeambulia nafasi 3211 ambapo kati ya nafasi hizo, Chadema pekee imepata 2001, CUF 1181 na nafasi 29 zilizosalia zimekwenda kwa vyama vidogovidogo vya upinzani ikwemo NCCR-Mageuzi.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Mafanikio hayo kwa Chadema, na kushindwa huko kwa CUF, kumeelezwa ni matokeo ya vyama hivyo kuzunguukana kisiasa ndani ya
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA [/FONT]kwa kila kimoja kutaka kukipiku kingine na kushika namba mbili nyuma ya CCM katika uongozi wa vyama vya siasa nchini ili hatimaye kitambulike kama chama kikuu cha upinzani.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Wakati Chadema kikitajwa kupata mafanikio hayo kupitia mwavuli wa umoja wa
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT] uliyokisaidia kwa kiasi kikubwa kupenya ngome ya CUF na kuzoa wafuasi kadri ilivyotaka, CUF yenyewe imeelezwa kuwa iliathiriwa na viongozi wake kubweteka kwa kutokufanya kampeni kabambe kama kawaida yao katika uchaguzi huo ikitegemea mbeleko ya [/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT] kupata mafanikio.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Aidha kitu kingine kinachotajwa kuiathiri CUF katika uchaguzi huo, ni kitendo cha viongozi wake kuruhusu viongozi wa kitaifa wa Chadema kuingia katika ngome zake hasa zilizopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam, na baadhi ya maeneo ya kanda ya Magharibi na Ziwa na kufanya kampeni ya kuwarubuni wafuasi wa CUF kwa kuwataka kuiunga mkono Chadema kwa kisingizio cha vyama hivyo kuwa katika umoja wa
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT].[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifanya kampeni nzito kwa kutumia Chopa akiwashawishi wafuasi wa
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT] wakiunge mkono chama chake katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kisha akafuatiwa na Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa ambaye naye alitumia staili ileile kuwavuta wafuasi wa UkAWA kujiunga na Chadema.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Katika mikutano hiyo ya hadhara ya viongozi wa kitaifa wa Chadema iliyofanyika karibu nchi nzima wiki chache kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika, Mbowe na Dk. Slaa walikuwa wakipigia debe zaidi chama chao cha Chadema na si
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT].[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Hali hiyo ni tofauti na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye kwa nyakati tofauti alipofanya ziara katika ngome yake ya mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara), na baadaye nyumbani kwao Tabora, alitumia muda mwingi kutangaza na kusisitiza juu ya umuhimu wa kushikamana katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT]) kwa manufaa ya siasa za mageuzi, badala ya chama kimojakimoja cha siasa kikiwemo chama chake cha CUF, pengine alifanya akiamini kuwa viongozi wenzake katika umoja huo wana dhamira nzuri katika ushirikiano huo.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Kutokana na kuzunguukana kwa viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kulikoonekana mapema katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji mwaka huu, baadhi ya wanasiasa wametabiri mwisho mbaya wa umoja huo unaundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na DP.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Kuzunguukana huko ndani ya UKAWA, kumefurahiwa na baadhi ya wanasiasa wa chama tawala, CCM ambapo mmoja wa makada wa chama hicho, Amina Makilagi ameonya kuwa ikiwa Chadema kitaendelea na janja yake ya kuvizunguuka vyama vingine vya upinzani vinavyounda
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT], ni wazi kuwa umoja huo hautakuwa na maisha marefu.[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Makilagi ambaye alikuwa akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita na moja ya chombo cha habari hapa nchini akiwa nchini Qatar katika ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema kutokana na matokeo ya uchaguzi huo yalivyotangazwa huku yakionyesha vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi kufanya vibaya kulinganisha na matokeo ya mwaka 2009, ni kama vyama hivyo havipo tena kwenye ushindani wa kisiasa.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
“Hawa Chadema ni wajanja sana, angalia walichopata wao, halafu angalia na walichopata CUF na NCCR-Mageuzi. Ni ujanja ujanja tu, Chadema ndiyo inayojitangaza kuliko vyama vingine katika Ukawa”, amenukuliwa Makilagi ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Ikumbukwe kuwa kabla ya kuwepo kwa UKAWA, CUF ilionekana kufanya vizuri kisiasa kuliko vyama vingine vya upinzani katika pande zote za Muungano, yaani Tanzania Bara, na Tanzania
Visiwani kiasi cha kuitwa chama kikuu cha upinzani baada ya kushika namba mbili, nyuma ya CCM.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
CUF kabla ya kupinduliwa
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji uliyofanyika mwaka 2009, CUF ilipata nafasi 540 huku Chadema ikiambulia viti 413 na NCCR-Mageuzi 39, hivyo kuifanya CUF kuongoza vyama vya upinzani.
[/FONT]
[FONT=Times,"Times New Roman",serif]
Kutokana na mafanikio hayo ambayo CUF ilipata mwaka 2009 dhidi ya Chadema, na kuanguka kwake mwaka huu katika uchaguzi huo, ni wazi kuwa wakati Chadema ikifurahia ushindi wake huku ikidai ni ushindi wa
[/FONT][FONT=Times,"Times New Roman",serif][FONT=Times,"Times New Roman",serif]UKAWA[/FONT], CUF kwa upande wake inaugulia maumivu ya kisiasa kwa chama hicho kupoteza muelekeo hasa kwa upande Tanzania Bara. [/FONT]
 
Fitina hizi haziwezi kuzaa matunda! Hangaikeni na yale ya wazee wa Dar Es Salaam jinsi walivyomzomea Mwenyekiti wa Chama chenu na kumfanya aseme, "Napata kikohozi!"
 

samahani kwa kuquote li uzi lote but huu uzi si mahala pake hapa peleka jukwaa la siasa, pili fitna zenu zinajulikana
 
Hivi waandazi wenginr wa thread huwa wanatafakari kabla ya kuzirusha au...!!!???

Hiki kingekuwa kipindi bora kabisa cha kujadili ufisadi unaoitafuna nchi na kutafuta njia za kuliondoa taifa katika mikono ya manguruwe...

Mtoa thread umetumwa kufanya fitina juu ya Ukawa...

Umewahi tafakari ccm imepoteza mitaa, vijiji na vitongoji vingapi...!!??

Tafakari...
 
Kweli mtoa mada una lako jambo kwani km Cuf mwaka 2009 viti 540 na mwaka huu 1181 hapo wamepoteza wamepata?? Acha kwenda kichwaa kichwa hivyoo we we umetumwa na Ccm kwa hofu yenu juu UKAWA na mtakiona tu kwa kifupu Ccm wameshinda kwa 47% kura ya kupigwa na mapingamizi 33% wait 2015 time will tell
 
Waswahili wanasema "Kapo la mchaga Mpemba hatii Mkono".
 
Fitina hizi haziwezi kuzaa matunda! Hangaikeni na yale ya wazee wa Dar Es Salaam jinsi walivyomzomea Mwenyekiti wa Chama chenu na kumfanya aseme, "Napata kikohozi!"

We ndio zuzu kwelikweli.
 
Acheni fitna kutaka kuwagawa wana-ukawa, 2015 siyo mbali wananchi wanachukua nchi yao.
 
Ukawa haiwezi kusambaratika kwa analyis za vichwa maji kama hawa. Who is Makilagi by the way? ana credibility gani ya kuweza kuwa mchambuzi wa siasa?
 
J.inga kweli.... UKAWA hawashindani wao kwa wao....ushindi wa Chadema ni ushinsdi wa ukawa,ushindi wa CUF ni ushindi wetu sote.
 
Hii ni propaganda ya kuwagawa ukawa.
 
Ndio hivyo ilivyotakikana tuungane tuwe kitu kimoja ,sasa kama hatukufunikana miiccm si ingelituona tulipo ,,Unajua hapa mlipo maccm mmepata nusu wazimu ,maana hata kumfukuza Anna kwa kutumia wazee wa DSM inaonyesha kabisa mmeshavurugika ,tatizo mkisikia kuwa sasa UKAWA wanaungana kuwa Chama kimoja naamini bila ya shaka yeyote ile mtapata wazimu kamili.
 
Username: Upanga mkali
join date : Today 24th december 2014.

Kametumwa na nape haka kuja kusambaza propaganda za kugawa ukawa, kwa taarifa yako kamwambie nape kuwa ukawa haitatengana kamwe .
 
Username: Upanga mkali
join date : Today 24th december 2014.

Kametumwa na nape haka kuja kusambaza propaganda za kugawa ukawa, kwa taarifa yako kamwambie nape kuwa ukawa haitatengana kamwe .
Asante kwa taarifa hii...we ni mkweli
 
 
Cc:- upangamkali.
Mbinu unayotaka kuitumia ya kutoa data za uongo juu ya ukawa ziliumaliza umoja wa soviet(ussr). Ni aibu kwa mtu uliyekwenda shule ambayo imekusaidia kubaki mjini kuitetea na kuisemea ccm pamoja na ufisadi wote unaoujua kuwa unafanywa na viongozi wakuu wa ccm. Hebu jiulize, chama chako ccm kinakuongoza kuelekea wapi zaidi ya umaskini street?. Na wewe umekaa tu unawapigia makofi hata pale wanapojamba kwa kuvimbiwa fedha za escrow. Huwaonei huruma japo si hulka yenu ccm, nduguzo wanaotaabika vijijini na hata hapo ulipo kwa kukosa huduma za msingi?. Hizi buku 7 zitawatoa nyongo 2015. Waache ukawa wapige mzigo kwani nape na kinana wako wapigwa singi hata kabla hawajashuka jukwaani kwa kuwaongopea wananchi. Wanampinga mwenyekiti wao waziwazi. Sijui hakuna collective responsibility huko ccm!.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…