Hali ya CHADEMA yaanza kuteteleka kata ya Mbezi baada ya mapandikizi ya CCM na ACT ndani ya CDM kuanza kubungua taratibu. Mamluki hao wakiongozwa na Makweta (aliyejiunga na CDM akitokea CCM) kufurukuta hadi kupata uenyekiti chama wa mtaa Makabe.
Nafasi ya mwenyekiti ameipata baada ya kuendesha na kupiga majungu yaliyomlazimisha mwenyekiti aliyekuwepo kujiuzulu.
Makweta na kundi lake wamefanikiwa kuuweka mfukoni uongozi wa chadema Kata ya Mbezi Luis na Jimbo la Ubungo. Uongozi wote wa Chadema Jimbo na kata kwa sasa wanacheza ngoma inayopigwa na Makweta.
Kwa sasa, katiba imekuwa ikivunjwa wazi wazi ili mradi Makweta na mamluki wenzake wafanikishe malengo yao. Lengo mojawapo,ni kuhakikisha wanapandikiza watu wao kwenye ngazi za juu za chama katka kata ya Mbezi Luis. Hadi sasa wamelazimisha uchaguzi ndani ya chama urudiwe kwa kujaza nafasi zote. Wamelazimisha kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi za wazi na kuwaondoa hata viongozi waliopo na waliochaguliwa mwaka jana.
Jambo lisiloeleweka ni pale ambapo viongozi wa kata na jimbo wanaendesha chaguzi zilizoamriwa na Makweta; huku wakijua dhahiri kwamba baadhi ya nafasi zinazoitiwa uchaguzi zina viongozi wanaozishikilia tangu uchaguzi wa mwaka jana.
Lengo la kupandikiza mamluki likikamilika, mkakati ufuatao ni kumng'oa mwenyekiti wa serikali ya mtaa (kwa tiketi ya Chadema) mtaa wa Makabe. Mkakati huu ni kuhakikisha uchaguzi uchaguzi serikali ya mtaa unarudiwa ili CCM waushike mtaa tena.
Makweta na kundi lake,wamepanga kufanya mafarakano na mtifuano ndani ya chadema kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 ili kuweka mazingira mazuri kwa mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM kupita.. Kwa sasa kata ya Mbezi ina diwani kupitia CHADEMA mh.Kagale. Hilo ndilo lengo mahususi la Makweta na mamluki wenzake ndani ya CDM.
Makweta amekaa kimkakati ili kuweza kupata donge nono la fedha na cheo kikubwa ndani ya chama cha CCM.