CHADEMA wana umoja japo hawafahamiani

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Kwa namna maisha yalivyo magumu na kwa muda uliotumika kukusanya milioni tano zakumwepusha Yeriko Nyerere na kifungo, nakiri kuwa Hawa watu wanaumoja usiomithilika.

Lisaa limoja kupata 5M kwa tangazo la tweeter, Instagram na Facebook itoshe kusema mizizi hii imejikita kwenye shina la miyoyo ya watu. Niwaombe wailinde imani hii waliyopewa. Imani ya waliohama kufa kisiasa na waliobaki kupanda chati kisiasa.

Karibu uraiani Yeriko Nyerere mzee wa mizimu
 
Ni kweli. Wengine wako kulekule CCM...

Yaani wanakula CCM, lakini mioyo yao yote iko CHADEMA...

CHADEMA ni Yuda au Israel...

Hii hofu iliyoko kwenye kambi ya Wafilisti (CCM) inatokana na nguvu ya umoja huu...

Wanajua hili na kila mmoja anajua kwelikweli...
 
Propaganda hizo wewe, pesa walikuwa nayo. Hiyo kuchangisha ndani ya saa 1 ni propaganda, shtuka.
 
Tumeonya mara kadhaa kwamba Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 
Na CHAUMMA tuna umoja pia. Kwa kuuenzi umoja wetu hua tunakula ubwabwa angalau mara moja katika siku mbili.
 
Propaganda hizo wewe, pesa walikuwa nayo. Hiyo kuchangisha ndani ya saa 1 ni propaganda, shtuka.

Nadhani una hasira na jambo hili! Ukisoma vizuri mada utaona kinachozungumziwa pia ni huo moyo wa kuchanga wakiwa hawajuani!

Au una maanisha milioni 5 ni pesa nyingi sana? Bahati nzuri hujakanusha kuchangwa kwa pesa hizo!
 
Hata sisi wateja wa vitabu vya Yericko na wale majirani tumemchangia bila kujali tofauti zetu za kiitikadi.

Kuna maisha baada ya siasa bwashee!
Hivi umeiacha kauli mbiu yako ya maendeleo hayana chama?
 
CHADEMA imekaa ki saccos - saccos tu. Mil 5 ilitakiwa siku ya hukumu hela inakuwepo mfukoni, sio mambo ya kuchangachanga.
Yeriko anauza mavitabu anakosa mil 5?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…