CHADEMA wamvaa Kamhanda

SIMON CONDRAD

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
9
Reaction score
10
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Mkoa wa Iringa, limeelezwa kusikitishwa-na kitendo cha Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael-Kamuhanda kujivika jukumu la kupachika raia vyeo ambavyo haviko kwenye utaratibu wa chama.

Kauli ya CHADEMA imekuja siku moja baada ya Kamanda Kamuhanda kudai kuwa mtuhumiwa wa ujambazi aliyekamatwa mkoani humo, Athanas Mongo ni Kamanda wa Vijana wa chama hicho mkoani Iringa

Taarifa ya Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Joseph Lyata kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa Kamuhanda alipotosha umma kwa kumpachika cheo bandia mtuhumiwa huyo ili kutimiza lengo la kujaribu kukipaka matope CHADEMA.“Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zilizotolewa na Kamuhanda si za kweli kwani mtuhumiwa wa ujambazi si Kamanda wa BAVICHA Mkoa wa Iringa na wala muongozo wa mabaraza ya chama unaosimamia mabaraza yote hautambui cheo hicho,” alisema.

Lyata alisema kuwa wanavyofahamu wao, cheo hicho hutumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).“Mongo-ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA asiye na cheo chochote-ndani ya chama.

Ni Mtanzania mwenye haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Kutuhumiwa kwake kwa masuala ya uhalifu hakupaswi wala hakuwezi kuhusishwa na-chama chake,” alisema.

Alisema kuwa BAVICHA wanamuonya Kamuhanda kuacha mara moja tabia ya kukurupuka na kutokuwa makini katika utendaji kazi-kiasi cha kuingilia na kujaribu kubaka Katiba-ya CHADEMA na kanuni za BAVICHA ili tu kukidhi haja yake ya kuwapaka matope.

Lyata aliongeza kuwa Kamuhanda anafanya hivyo baada ya kushindwa hila hizo kwenye tukio la mauaji ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi kule kijijini Nyololo.
 
Huyo Kamuhanda muuaji anafanya nini hadi sasa kwenye Ofisi ya Umma? Hana hadhi katika jamii kabisa huyo ni muuaji tuu na siku yake yaja ya kutafunwa na laana ya kumwaga damu ya watu wasio na hatia.
 
Huyo Kamuhanda muuaji
anafanya nini hadi sasa kwenye Ofisi ya Umma? Hana hadhi katika jamii
kabisa huyo ni muuaji tuu na siku yake yaja ya kutafunwa na laana ya
kumwaga damu ya watu wasio na hatia.
Mnakanusha nini kila mwanachama cdm ni kamanda, kwa hili muwe wapole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…