Kwanza lipo jambo lililowazi sana katika hoja yako....umechagua maelezo yanayokwepa mafanikio ya mabadiilo haujataja Africa ya Kusini baada ya fujo hadi Mandela kutoka gerezani....je kuna tofauti? Haujataja mabadiilo ya kiuongozi Ghana na mafanikio yake ... haujataja Mabadiliko Kenya .... nk.
Kwa kukupa mifano tu .... Chama kilichorpa madarakani Kenya kwa sasa hakijawahi kuwa hata na diwani kabla ya uchaguzi wa mwaka huu..... usichofahamu wewe ni Siasa, serikali siyo chama na chama hakiwezi kuwa serikali ila kinaomba ridhaa ya kuendesha serikali tu. Ndio maana inawezekana kuwa na mgombea huru hana haja ya kuwa na chama ilikuonyesha kimefanikiwaje
Na mwisho katika nchi hizo unazo seam zina fujo maudhui yake hazifanani na CDM....Misri, Tunisia, Libya kote huko wananchi waliamua yawepo mabadiliko lakini siyo chama kilichosajiliwa km CDM ambacho kinahamasisha mabadiliko ya kisheria.
Sijui kama umenielewa nimejaribu kujibu kifupi ila tatizo ulilonalo ni uelewa wa kisiasa tu ndio tatizo
Sasa hapo umeamua kujifunga wewe mwenyewe umetolea mfano wa Afrika Kusini, umeshafika Afrika Kusini wewe sasa hivi? mimi nimefika na nina rafiki zangu Walimu Port Elisabeth na wengi wanasema hakuna jipya lolote ANC ililofanya kwanza wanasema ukiongea na walalahoi kabisa wanasema ni bora hata wakati wa Wazungu kwamba walikuwa wanabaguliwa lkn kulikuwa na kazi hata za kufua nguo kwa Wazungu na mshahara ulikuwa unatosha kula angalau mpaka mwisho wa mwezi huu ni Ushuhuda ukifika Afrika Kusini utaupata, waliyoahidi yote ANC ni Usanii mtupu, Black empowerment programm ya Mbeki ni ya wachache kwa kifupi hakuna Mafanikio yoyote Afrika Kusini.
Ni hivi juzi tu hapa Serikali ya ANC imetumia Jeshi lile lile la Kikaburu na mbinu zile zilezile za kikaburu kuuwa watu wale wale waliokuwa miaka yote wanauliwa na Makaburu, Hivyo Afrika kusini sio success story!
Unaongelea Kenya unadaganya wazi wazi, mabadiliko ya Kenya wala huwezi kuyaita mabadiliko pasee kwa maana Viongozi wote ambao wanaongoza Kenya sasa hivi ni wale wale waliokuwa Kanu au CCM ya Kenya, ni kama leo hii akina Bw.Lowasa wahame CCM waingie Upinzani halafu washinde uchaguzi, nafikiri hauelewi siasa za Kenya, nitajie mafaniko ya Kenya ukilinganisha na wanakotoka, usinitajie Katiba mpya, niambie mwananchi wa Kenya wa sasa hivi anatofauti gani na wakati wa Moi? Maisha yamebadilika kwa kiasi gani?
Kuhusu Ghana sielewi mambo yao zaidi ya kujua tu walikuwa wanatawaliwa kijeshi!
Kurudi kwenye Mada yangu ni kwamba, nataka Chadema waonyeshe walichofanya, na sio kuniambia kwamba kutaja orodha ya Mafisadi ndio kunatosha kusema kwamba wao ni bora kuliko CCM, waseme kwa mfano kuna Halmshauri wanaziongoza, Je wamefanikiwa kwa kiasi gani ukilinganisha na Halmashauri zinazoongozwa na CCM usinitajie Moshi mjini, Moshi iko jinsi ilivyo kabla hata upinzani haujazaliwa Tanzania, yaani mimi kama mwananchi nataka niseme Halmashauri fulani mambo yake mazuri ukilinganisha na Halmashauri yangu kwa sababu inaongozwa na Upinzani, hiyo ndio baadhi ya mifano ninayoitaka kuiona, na sio sijui Lowasa fisadi na blah blah
[/QUOTE]
Sijui km wewe ni mwingi wa kujisomea naona uhaba mwingi sana wa ufikiri km point yangu ya Kenya unasema ni viongozi wale wale Mbowe, Slaa,Lisu wote walikua CCM sasa kma hilo ndilo unalolikubali kulikua na haja gani ya kuutaka ufafanuzi wa nini CHADEMA wamefanya kuonyesha uwezo wao ! kifupi tu nakujibu kwa stailli yako kuwa si walikuwa CCM wakahamia CDM?
Una hakika kuwa hakuna tofauti ya maendeleo ya watu kwa tathmini yako kuwa Afrika ya Kusini hii si bora kuliko ya makabu utu? Hebu tijikite ktk hili je ni kweli unayoyasema...., hivi ktk uelewa wako unadhani serikali ya sasa yenye kufuata misingi ya Demokrasia na ile ya Makaburu ya Ubaguzi isiyo na Demokrasia ndio yenye mwelekeo wa tija? hapa tena nikifuta uelewa wako huu haja hii itatakua imekufa kwani unataka kujua CDM imefanyika nini ktk mfumo wa kidemokrasia sasa km hauamini ktk Democrasia unawezaje ukayanyumbulisha wanayoyafanya CDM...? Mfano wako wa polisi Afrika ya kusini kutumia nguvu ni kweli ulitokea .... la kujiuliza je baada ya tukio baya vile serikali haikuwajibika kwa wananchi wake kisheria na je hatua za kisheria zililindwa...na je wakati wa Ubaguzi nani angeweza kupewa haki? Mwananchi? hii ndio tofauti ya kiutawala km ulishindwa kuona hili basi....!
Umerukia ya Kenya utafikiri umetumia umakini...eti kwakuwa Kenyata na baadhi ya viongozi walikuwa KANU basi inatosha kuwa na utayari wa kutawala mbona hausemi Mbowe, Dr. Slaa, Tundu Lisu na wengine walikua CCM hivyo wanao huo utayari wa siasa ...eti Kenyata chama chake si kipya kwa sababu hiyo hiyo ya yeye kuwepo KANU basi km hilo ndio uelewa wako unashindwaje kuamini CDM nao wana sifa km za JUBILE
Ghana vyama tofauti vimechukua maduara kwa kupotezana Leo fedha yao iko juu moja ya ishara za maendeleo
Ambacho CDM imekifanya kubwa ni kusimamia na kuzuia ufujaji wa fedha za uma..,hili limefanyika sana kwa namna moja au nyingine ktk halmashuri nyingi chini ya upinzani...nini maana yake km ufujaji utadhibitiwa makusanyo ya kodi ya mapato yatakuwa na tija hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la kodi ambazo hupunguza mapato ya wananchi na kuongeza uduni wa familia za kitanzania ... kazi ya kumlinda mwananchi wa chini hua haina muonekano wa wazi km ilivyo kwenye barabara za lami na maghorofa makubwa tumeaminishwa hayo ndiyo maendeleo sasa juhudi za kumjenga mwananchi hazitizamwi km juhudi za kimaendeleo.
Jingine ambako ndio baya kuliko ni hili la serikali kuu inayosimamiwa na CCM kushinikiza serikali za mitaa kutekeleza ilani ya uchaguzi ... Ukisoma kwa makini hata itikadi ya CCM yenyewe inataja kuwa .... ili serikali za mitaa ziweze kuyafikisha maendeleo kwa watu ni lazima kusiwepo mwingiliano kt ya serikali Kuu na serikali ya mitaa USIWEPO hata kidogo ... la ajabu, makusanyo ya kodi za halmashauri (serikali za mitaa au local governments) kwa u jumla wake zinapelekwa Serikali kuu ili zipangiwe matumizi na kubwa hapa ni fedha kwaajili ya utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ambayo mgombea urais aliahidi wakati huo huo madiwani nao wametengeneza maombi ya shughuli za kimaendeleo waliotumwa na wananchi wao sasa hapa mgongano na mvutano unaanza ... Rais anaweza kuahidi daraja Singida fedha zitatafutwa kodi itapanda magulioni ili hela ipatikane kujenga daraja... Mwananchi anakosa hamu ya kuyataka maendeleo kwani mzigo unakua mkubwa sana...Mwananchi anakata tamaa bado michango ya madarasa bado ya zahanati na yote hayo ni nje ya kodi inamuandama yeye tu.... anajikuta anajitoa saaana kwa serikali yake lakini kwa kuathiritija binafsi km mzalishaji mali huku fedha ambazo itoa zinatumika vibaya bila tija...huku lindi la umasikini kumkabili...bado kuna sera km "Kilimo kwanza" sera inayomnyang'anya mwananchi huyo huyo ardhi ambayo ndio chanzo cha mapato yake na kupewa wawekezaji wakubwa utaratibu ambao hata washirika wakubwa wa CCM nchi ya China haikuwa mafedhuli namna hii kwa watu wake. China iliwaunganisha hao hao wakulima wa dogo wadogo ikawapa malengo na Leo wanalisha watu zaidi ya bilioni 1.3, CDM inapambana kuyarekebisha haya....ili kumjenga Mwananchi awe chachu ya maendeleo bila hivyo Mwananchi atakua omba omba na mpuuzi yeyote akiweza kumpa hata maembe ale siku hiyo na familia yake atamchagu akidhani atakua anamlisha kila siku....hizi ndio kazi za CDM
Google.co.tz offered in: Kiswahili
Settings Help
View Google in: Mobile | Classic
Google.com
© 2013 - Privacy