Developing story...kutofautiana mikoani
Naye Katibu Mwenezi wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Matongo alisema kuwa kilichotokea ni msukosuko jambo ambalo ni kitu cha kawaida kwenye vyama vya siasa.
Hata gari linapokuwa katika safari huwa linakumbana na matatizo mbalimbali kabla ya kufika mwisho wa safari, hivyo kikubwa kwao ni kukaa meza moja ya mazungumzo, alisema Matongo.
Naye Erasto Jetha mkazi wa Mpanda alipongeza uamuzi wa Arfi akieleza kwa muda mrefu wamekuwa wakipuuzwa wanapotoa ushauri kuhusu kukiimarisha chama hicho.
Joseph Makumbule anasema kuwa Arfi ameonyesha uzalendo kwa kujiuzulu kwake hasa kwa wananchi wa Katavi.
Kigoma
Kutoka mkoani Kigoma, wakazi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini wametaka Zitto arejeshewe nafasi zake wakihofia mpasuko katika chama hicho.
Mmoja wa wakazi hao, Abdi Mtemi wa Kijiji cha Msiba alisema: Zitto arudishiwe nafasi yake ya unaibu katibu mkuu, nina hofu kuwa chama kitapasuka.
Naye Shabani Musa wa Kijiji cha Kigaza alisema kuwa chama ni zaidi ya mtu na kwamba anapongeza uamuzi wa Chadema huku akiungwa mkono na Atanas John wa Kamara aliyeeleza kuwa chama ndicho kinaamua, hivyo lazima viongozi waheshimu mamlaka .
Arusha
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha(Chadema), Joshua Nassari amesema kuwa anamsikitikia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa kuvuliwa nyadhifa, lakini akamtaka kujipanga upya akieleza kuwa bado ana nafasi ya kungara kwenye siasa za Tanzania akiwa Chadema.
Nassari alisema kuwa kilichomtokea Zitto ni jambo la kawaida katika siasa na bado anaweza kujipanga ndani ya Chadema na kufikia malengo yake. Tukio hili linatupa funzo kuwa hakuna mwenye uwezo zaidi ya chama kwani ndicho kimemfikisha alipo, lakini naamini Zitto ana uwezo wa kukiri makosa na kujipanga upya kwani bado ni kijana na bado ana nafasi ya kujipanga,alisema Nassari.
Alisema kuwa binafsi aliingia kwenye siasa kutokana na kuvutiwa na Zitto tangu akiwa Chuo Kikuu na anaamini kwamba safari ya Zitto haitaisha baada ya kuvuliwa uongozi.Akizungumzia sababu za kuvuliwa nafasi za uongozi, Nassari alisema kuwa ni sahihi akieleza kuwa haiwezekani kufuga nyoka mwenye sumu ndani ya nyumba.
Ni bora uwe nyikani ukijua kuna simba zaidi ya 10 kuliko kuwa ndani ya nyumba na nyoka mwenye sumu, alisema Nassari.
Mwanza
Kutoka mkoani Mwanza habari zinaeleza kuwa chama hicho katika Manispaa ya Bukoba Mjini kimepongeza uamuzi wa kuwavua nyadhifa zao viongozi hao wa ngazi za juu na kusema uamuzi huo unapaswa kuwa fundisho kwa viongozi wengine.
Kwa mujibu wa tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba Mjini, Victor Sherejey na Katibu Mwenezi, Peter Mweyunge, chama ni muhimu kuliko kiongozi na kwamba kila kiongozi anapaswa kuheshimu chama kupitia Katiba na siyo kuwa juu ya chama.
Tamko hilo lilifafanua kwamba hatua hiyo inapaswa kuigwa na vyama vingine vyenye tabia ya kuwalinda viongozi wake waovu.
Habari imeandaliwa na Gasper Andrew, Singida; Mussa Juma, Arusha; Frederick Katulanda, Mwanza; Anthony Kayanda, Kigoma na Mussa Mwangoka, Rukwa.