CHADEMA inavyoisaidia CCM kushinda kwa zaidi ya 98% uchaguzi ujao

Katiba mpya ni kisingizio tu yeye akishaadumbukia kwenye hizo ruzuku ndo basi tena zinazobaki ni porojo tu na ngonjera maukoto ndo swala la msingi
 
Bora mimi ninayejaribu na huko unakokuita wewe "kufeli."

Hiyo njia yako ya kusubiri "machafuko na mapinduzi", na yasipotokea unabaki tu hivyo hivyo na njia yako ya kuzira, kama mtoto anayejifanya kuzira kula cha kula, na akiachwa, anakuja mwenyewe kula bila kuhimizwa!
Unasusia uchaguzi, CCM anasherehekea ushindi wa chee kabisa, unaendelea kulialia hivyo hivyo na kusubiri vurugu au mapinduzi ambayo hayatokei.

CHADEMA hata siku moja hawajaweka juhudi za kufanya ninayopendekeza kwa ufanisi mkubwa. Ndiyo, ni kazi ngumu, lakini ni kazi inayowezekana kufanyika wakitaka kuifanya vizuri.

Hata hizo "vurugu na mapinduzi" na unavyovishabikia wewe, husemi vitaanzia wapi, unasubiri tu vitokee vyenyewe!
 

Narudia tena mkuu hizo njia zako zimeshafeli, ni wendawazimu kuendelea kushiriki chaguzi zisizoheshimiwa ukitegemea matokeo tofauti. Tujadili njia nyingine, sio hizo za kupotezeana muda. Na ukiona hao cdm hawafanyi utakavyo wape mbinu hizo chama kingine wazitumie kuing'oa ccm. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njia pekee. Imeisha hiyo.
 
Ukiacha chadema watu mtaani wanaona 24/25 iwe kesho ili waipeleke CCM ilipokwenda TANU uzee wa CCM unaigharimu Tanganyika
 
Zilijaribiwa lini na wapi zikafeli?

Lakini hapo ulipo, siku zote unaimba wimbo huo huo wa "vurugu na mapinduzi", lakini hata kueleza yatatoka wapi huwezi!
 
Zilijaribiwa lini na wapi zikafeli?

Lakini hapo ulipo, siku zote unaimba wimbo huo huo wa "vurugu na mapinduzi", lakini hata kueleza yatatoka wapi huwezi!
Mkuu anzisha chama utumie hizo mbinu zako uchukue nchi. Mimi naamini kwa tulipofikia machafuko au mapinduzi Pekee ndio yataleta mabadailiko, sio hiyo njia ya kura kwa hizo mbinu zako za kinadharia zaidi. Yatatokeaje hilo ni jambo jingine. Na hayo mipango yake sio ya hadharani.
 
Mimi sijakuona hata siku moja ukifanya mipango ya kuanzisha vurugu, wala kwenda pahusika kuamru kufanyike mapinduzi; lakini unakuwa na uthubutu wa kuja hapa na kunitaka nianzishe chama?
Mbona unazidi kuwa mtu wa hovyo kiasi hiki?

Unajitoa ufahamu kweli kweli unapohimiza mapinduzi upande mmoja, halafu hapo hapo unasahau kuwa hao unaowalilia kuleta mapinduzi ndio hao hao unaolalamika kutumiwa na CCM kuwafanya wabaki madarakani..

Unataka vurugu zianzishwe na akina nani, wakati huo huo waTanzania hao hao unawalalamikia kuruhusu kutopambana na 'Dola' inayotumiwa na CCM kuwabakisha madarakani?

Sasa hao watakaoleta vurugu na mapinduzi wrewe umewaficha wapi, na wanasubiri hadi lini ndipo uwaamrishe wafanye hayo unayotegemea wewe?
 


Hakuna nchi ya Demokrasia chama kimoja kinashinda 90% ukiona hivyo ujue hakuna demokrasia na wala usisingizie Chama. Angalia USA, Canada na hata Kenya kwenye demokrasia kupata zaidi ya 60% ni ngumu. Ukiona uchaguzi msindi ana 60% kama Tanzania ni kwasababu ya wizi wa kura ambao kila mtu hata waangalizi huru walisema 2020!. Hiki sio kitu cha kujivunia kabisa na ni aibu maana ni maendeleo yetu na wajukuu zetu ndiyo yanaumia
 
Bro acha kupanick, mbinu zako zimeshafeli. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njia Pelee ya kuleta mabadaliko ya kweli hapa nchini. Kufanyika ama kutofanyika hilo ni jambo jingine. Mapinduzi hayaletwi ni viongozi wa dola, bali wa vyeo vya chini.
 
MAPANZI YAKIWA YANAZIPIGA KUNGURU ANA KAZI MOJA TU NI KUYATAFUNA YOTE KWA PAMOJA
Kwahiyo ndio unaishaur chadema hivyo.....yaani tuache ajenda ya chadema digital....chadema ni msingi....chadema grassroot na uchaguz ndani ya chama na kusajiri wanachama upya kielectronic tukimbizane
 
Bro acha kupanick, mbinu zako zimeshafeli. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njia Pelee ya kuleta mabadaliko ya kweli hapa nchini. Kufanyika ama kutofanyika hilo ni jambo jingine. Mapinduzi hayaletwi ni viongozi wa dola, bali wa vyeo vya chini.
Mtu mwenye akili safi kabisa unapoamua kwa maksudi kabisa kukomalia jambo ambalo wewe mwenyewe unaona wazi kuwa halipo, watu wanaokufahamu itabidi wabaki tu wakikushangaa.

Sioni chochote unachokomalia hapa, mbali ya kuona tu aibu kukubali kwamba unachong'ang'ania hakina maana yoyote.
 
Yaani nione aibu kwa kutoamini unachoamini ww? Au ww ndio SI Unit ya aibu Nini? Ninachoamini sihitaji kuungwa mkono na ww au wengi wa aina yako. Huo ndio ukweli ninaoamini baada ya hizo nadharia zako kufeli. Imeisha hiyo.
 
Yaani nione aibu kwa kutoamini unachoamini ww? Au ww ndio SI Unit ya aibu Nini? Ninachoamini sihitaji kuungwa mkono na ww au wengi wa aina yako. Huo ndio ukweli ninaoamini baada ya hizo nadharia zako kufeli. Imeisha hiyo.
Inaonyesha hata maana ya maneno hujui, ila unayatumia tu hivyo hivyo.

Kuna nadharia ipi katika mapendekezo niliyotoa CHADEMA wayafanyie kazi? Hapo kuna "nadharia" yoyote, katika kutekeleza mambo ambayo yapo wazi?

Umekomalia "vurugu na mapinduzi" siku nyingi humu, na huoni njia ya kukana mawazo ya hovyo kabisa kama hayo. Lililobaki kwako ni kung'ang'ania tu hivyo hivyo.

Siwezi kuunga mkono dhana potofu kma hiyo unayoishikiria wewe. Ni potofu, na usitegemee hata siku moja kuona jambo kama hilo likitokea ndani ya nchi yetu.

Mabadiliko yatafanyika, na CCM itasalimu tu amri wananchi watakapoamua kufanya hivyo. Kinachosubiriwa ni kupata viongozi makini wanaoweza kuongoza juhudi za wananchi wenyewe. CHADEMA wasipokuwa tayari kuifanya kazi hiyo, atapatikana mwingine, hilo usiwe na mashaka nalo kabisa.

Hata huko ndani ya CCM yenyewe kunaweza kutokea viongozi wanaoweza kusimamia mabadiliko hayo; kwa hiyo CHADEMA si pekee anayeweza kuifanya kazi hiyo.
 
Kwanza kabisa Mbowe atoke kwenye hiko kiti ni muda wa watu wenye misimamo kama wakina John Heche wapewe kiti. Nakuahidi wakifanya hivyo ikifika January 2024, CCM itakuwa inakimbiwa na wanachama wake jinsi huku uraiani patakuwa hapakaliki.
 
Mnaweweseka sana na chadema.mara imekufa,mara imejimaliza,mara haina agenda,mara inaisaidia ccm.hivi nyie watu mbona hamujielewi.hizo ni dalili za kuweweseka.Ambao hamuipendi chadema ndio mnaoanzisha hizi mada mbovu zisizoeleweka lengo lenu nikuona cdm ikivurugika baada ya sasa kuwaona wako kwenye mstari sahihi.mtaangaika sana.Wananchi wenye akili timamu tunaielewa cdm nyie wengine endeleeni kuweweseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…