Unstoppable
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,046
- 384
Mi nina wasiwasi na serikali yetu..
Kulazimisha waziri ajiuzuru inatokana na waziri huyo kushindwa kuifanya kazi alokabidhiwa kama alivyoeleza waziri, haina maana ndio suluhisho isipokuwa ndio mfumo wa utawala bora (Zero tolerance) ktk uwajibishaji wa viongozi wetu. Kama alivyotakiwa waziri mkuu Pinda kujiuzuru aliposhindwa kuwawajibisha mawaziri walioshindwa kazi zao ama kujiuzuru kwa mawaziri walishindwa kutekeleza wajibu na rais alifikia kubadilisha baraza la mawaziri ingawa yote haya hayakuwa suluhu ya matatizo yaliyopo.
Unaanza na Uwajibikaji ktk kurekebisha mamlaka kisha anatafutwa kiongozi anayeweza kusimamia kero na matatizo yaliyopo hasa kuhakikisha jumuiya na asasi za kidini haziwezi kutengeneza fitna ya kijamii kwa kutumia misikiti au makanisa wakati huo huo serikali nzima ikitafuta suluhisho. Kero hazitakwisha ndio mfumo wa maisha ya binadamu na hata hao Marekani wana kero ktk nyanja zote za maisha na ndio hapo umuhimu wa elimu inapochukua nafasi kubwa.
Lakini muhimu zaidi ni mtazamo wa kiongozi wetu Mzanzibar na Muislaam ktk swala zima la madsai ambayo binafsi yangu nina hakika majibu yapo palepale nyumbani haikuwa na haja wala sababu ya kumtafuta mchawi toka bara kufikia kuchoma moto makanisa kisha wakane hawakuhusika lakini wakati huo huo wanajisifu kwa msimamo wao na waliyoyafanya nyuma ya pazia la dini.
Hata huyo Allah hutazama na kuyawezesha yaliyo mema hata kama hufanywa na kafir na Sheitan humshawishi hata muumini kutenda yasiyo mema. Hakuna binadamu aliyehai alopigwa mhuri wa utakatifu kwetu sote tupo ktk mtihani mkubwa wa kiimani kwa yale tunayoyafanya kila siku ya uhai wetu. Hivyo kwanza ni makosa makubwa sana kwa kiongozi wa serikali au muumini kuweka dhana na watu waliofanya kitendo kibaya cha kuchoma moto kuwa sii Waislaam au wanazuo wa UAMSHO kwa visingizio vya Usalama wa Taifa wakati hakuna ushahidi lakini zipo sababu nyingi sana zinazopelekea makanisa kuchoimwa na waumini wenye chuki wakiitwa ati wenye siasa kali.
Tume ya katiba, Hakuna mtu anayechukua njia za mkato isipokuwa hawa walalahoi wanaoukataa Muungano ndio wenye kutafuta njia za mkato. hata Bara leo tukianzisha Kongamano utawaona watu wenye hasira na yaliyotokea Zanzibar, wana hasira na matusi mazito yanayoletwa na wahuni ambao hawakushiriki wala kuyaunga mkono Mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar. Nimeziona video nyingi sana acha hii moja au mbili za majuzi, na watazame watu wenyewe wakijiita Ustadhi utajua kwamba ni NJAA tu ndio inawasumbua wala sii Muungano japokuwa wanapenda sana kutumia Uzanzibar kana kwamba sisi Bara hatuna Uraia.
Hawa watu hawawezi kukwambia hata jambo MOJA ambalo linawakandamiza Wazanzibar ktk UHURU, HAKI na USAWA dhidi ya WABARA isipokuwa umaskini ulokiuka kutokana na uongozi mbaya wa CCM na sasa hivi CUF. Wasomi wao wengi wamekwazwa tu na muundo wa Muungano kuwepo kwa serikali mbili chini ya kuunda Moja, jambo ambalo linatushinda hata sisi waislaam kuelewa Utatu mtakatifu, lakini bila kufahamu kwamba ya kwamba mfumo huo ndio ulolinda kuwepo kwa Zanzibar hadi leo. Tukiunda nchi mbili, serikali mbili chini ya moja ya Kitaifa amini maneno yangu Zanzibar kama nchi na jina lake ndio litakufa kweli na kabla ya kufa Wazanzibar watataka tena kujitenga kabisa ikiwa swala ni kuvunja muungano. Na ikumbukwe tu historia ya nchi hiyo kuuvunja muungano ni jambo ambalo HALIKUBALIKI. Mtoto hawezi vunja ndoa ya baba na mama kwa mapenzi yake hata siku moja na hata ikija vunjika basi ni maamuzi ya baraza la Mapinduzi.
Ila inawezekana kabisa ndani ya mgogoro huu tukalipata suluhisho na binafsi yangu ningewaomba viongozi wetu wa bara na Zanzibar kuja hapa Canada wajifunze kutokana na muungano wa nchi hii maana unafanana sana na Tanzania ambako sehemu kubwa ya nchi hii ni Waingereza na sehemu ndogo ya Quebec ni Wafaransa na wamekuwa na kero kwa muda mrefu lakini sasa wamefikia suluhisho japokuwa bado Waquebec wanataka kujitenga kutokana na kuwa chini ya Milki ya Malkia maana wao na Malkia wana na historia ndefu ya uadui. Sisi hatujawahi kuwa na uadui huo na ppengine ni mdugu zaidi ya muungano wenyewe kwa sababu historia ya nchi hii inajieleza wazi kwambza hata hiyo Zanzibar inayodaiwa sio Zanzibar nzima, kesho wanaweza dai mikoa yote ya pwani including Malindi, Lamu na Mombasa kuwa sehemu ya nchi hiyo. Hivyo kukubali kuvunja muungano ni mwanzo wa kujenga matatizo mengine ambayo yatatokana na historia ya dini na utawala wa Sultan.
Haya ndio majibu yanayotakiwa kutoka kwa kiongozi Mzanzibar ambaye ni mjumbe wa baraza la Mapinduzi, na sii kuendelea kutukashifu kana kwamba sisi Wabara hatumtegemei Allah ktk matatizo yetu. Kusema kweli serikali lazima iwe makini sana na haya makundi ya hizi jumuiya za madhehebu ya dini yanayojitokeza kuchochea serikali za ubaguzi na hata kuzikosoa imani za dini kwa matakwa ya tafsiri zao wenyewe.
Ndibalema, Hivi CCM bado ipo au limebaki jina tu?Hivi kuna CCM ngapi humu nchini?
No No No, uzoefu unaonyesha tunaelekea BOKO HARAM na Alshababu, busara ni kukifuta kwani kufutwa kwake hakuzui wao kuukataa Muungano, maana sio lazima uwe chini ya kivuli cha UAMSHO ndo uukate Muungano.Mnaacha kuangalia mzizi wa tatizo, mnatafuta simple and cheap solution.
Wakati wa rasimu ya katiba tuliona yaliyomtokea sitta, na wala haikuwa uamsho, vikundi vya jamii mbali mbali vilialikwa rasmi, lakini ukitazama zile video kila aliyesimama aliongea kwa jazba na mwisho ni kuukataa muungano tena kwa hasira, Kuna mwanajeshi mstaafu alilia.
Busara zinahitajika sana naamini, sio kufuta usajili.
Kulazimisha waziri ajiuzuru inatokana na waziri huyo kushindwa kuifanya kazi alokabidhiwa kama alivyoeleza waziri, haina maana ndio suluhisho isipokuwa ndio mfumo wa utawala bora (Zero tolerance) ktk uwajibishaji wa viongozi wetu. Kama alivyotakiwa waziri mkuu Pinda kujiuzuru aliposhindwa kuwawajibisha mawaziri walioshindwa kazi zao ama kujiuzuru kwa mawaziri walishindwa kutekeleza wajibu na rais alifikia kubadilisha baraza la mawaziri ingawa yote haya hayakuwa suluhu ya matatizo yaliyopo.
Unaanza na Uwajibikaji ktk kurekebisha mamlaka kisha anatafutwa kiongozi anayeweza kusimamia kero na matatizo yaliyopo hasa kuhakikisha jumuiya na asasi za kidini haziwezi kutengeneza fitna ya kijamii kwa kutumia misikiti au makanisa wakati huo huo serikali nzima ikitafuta suluhisho. Kero hazitakwisha ndio mfumo wa maisha ya binadamu na hata hao Marekani wana kero ktk nyanja zote za maisha na ndio hapo umuhimu wa elimu inapochukua nafasi kubwa.
Lakini muhimu zaidi ni mtazamo wa kiongozi wetu Mzanzibar na Muislaam ktk swala zima la madsai ambayo binafsi yangu nina hakika majibu yapo palepale nyumbani haikuwa na haja wala sababu ya kumtafuta mchawi toka bara kufikia kuchoma moto makanisa kisha wakane hawakuhusika lakini wakati huo huo wanajisifu kwa msimamo wao na waliyoyafanya nyuma ya pazia la dini.
Hata huyo Allah hutazama na kuyawezesha yaliyo mema hata kama hufanywa na kafir na Sheitan humshawishi hata muumini kutenda yasiyo mema. Hakuna binadamu aliyehai alopigwa mhuri wa utakatifu kwetu sote tupo ktk mtihani mkubwa wa kiimani kwa yale tunayoyafanya kila siku ya uhai wetu. Hivyo kwanza ni makosa makubwa sana kwa kiongozi wa serikali au muumini kuweka dhana na watu waliofanya kitendo kibaya cha kuchoma moto kuwa sii Waislaam au wanazuo wa UAMSHO kwa visingizio vya Usalama wa Taifa wakati hakuna ushahidi lakini zipo sababu nyingi sana zinazopelekea makanisa kuchoimwa na waumini wenye chuki wakiitwa ati wenye siasa kali.
Tume ya katiba, Hakuna mtu anayechukua njia za mkato isipokuwa hawa walalahoi wanaoukataa Muungano ndio wenye kutafuta njia za mkato. hata Bara leo tukianzisha Kongamano utawaona watu wenye hasira na yaliyotokea Zanzibar, wana hasira na matusi mazito yanayoletwa na wahuni ambao hawakushiriki wala kuyaunga mkono Mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar. Nimeziona video nyingi sana acha hii moja au mbili za majuzi, na watazame watu wenyewe wakijiita Ustadhi utajua kwamba ni NJAA tu ndio inawasumbua wala sii Muungano japokuwa wanapenda sana kutumia Uzanzibar kana kwamba sisi Bara hatuna Uraia.
Hawa watu hawawezi kukwambia hata jambo MOJA ambalo linawakandamiza Wazanzibar ktk UHURU, HAKI na USAWA dhidi ya WABARA isipokuwa umaskini ulokiuka kutokana na uongozi mbaya wa CCM na sasa hivi CUF. Wasomi wao wengi wamekwazwa tu na muundo wa Muungano kuwepo kwa serikali mbili chini ya kuunda Moja, jambo ambalo linatushinda hata sisi waislaam kuelewa Utatu mtakatifu, lakini bila kufahamu kwamba ya kwamba mfumo huo ndio ulolinda kuwepo kwa Zanzibar hadi leo. Tukiunda nchi mbili, serikali mbili chini ya moja ya Kitaifa amini maneno yangu Zanzibar kama nchi na jina lake ndio litakufa kweli na kabla ya kufa Wazanzibar watataka tena kujitenga kabisa ikiwa swala ni kuvunja muungano. Na ikumbukwe tu historia ya nchi hiyo kuuvunja muungano ni jambo ambalo HALIKUBALIKI. Mtoto hawezi vunja ndoa ya baba na mama kwa mapenzi yake hata siku moja na hata ikija vunjika basi ni maamuzi ya baraza la Mapinduzi.
Ila inawezekana kabisa ndani ya mgogoro huu tukalipata suluhisho na binafsi yangu ningewaomba viongozi wetu wa bara na Zanzibar kuja hapa Canada wajifunze kutokana na muungano wa nchi hii maana unafanana sana na Tanzania ambako sehemu kubwa ya nchi hii ni Waingereza na sehemu ndogo ya Quebec ni Wafaransa na wamekuwa na kero kwa muda mrefu lakini sasa wamefikia suluhisho japokuwa bado Waquebec wanataka kujitenga kutokana na kuwa chini ya Milki ya Malkia maana wao na Malkia wana na historia ndefu ya uadui. Sisi hatujawahi kuwa na uadui huo na ppengine ni mdugu zaidi ya muungano wenyewe kwa sababu historia ya nchi hii inajieleza wazi kwambza hata hiyo Zanzibar inayodaiwa sio Zanzibar nzima, kesho wanaweza dai mikoa yote ya pwani including Malindi, Lamu na Mombasa kuwa sehemu ya nchi hiyo. Hivyo kukubali kuvunja muungano ni mwanzo wa kujenga matatizo mengine ambayo yatatokana na historia ya dini na utawala wa Sultan.
Huwezi kufananisha muungano huo na huu feki hata kama unaona kwako wewe uko sawa lakini kwa wataalam kam J. Ulimwengu huu si muungano ila ni muumizano. Muungano ulikuwa mwisho ni 1974 lakini Nyerere (LTLLAH) alipoona Karume anataka nchi yake alimmaliza kwa kumuua kwa risasi na mwaka 1977 alinza kuhodhi kila kitu cha Z'bar. Napia Aboud Jumbe alipojaribu kujitutumua kutaka kujitoa ktk muungano alivuliwa uanachama na kumvua uraisi na kumfunga kifungo cha ndani mpaka amezeeka, alafu unasema muungano huu ni sawa na wa Canada hapo umepotea kaka tafuta ukweli usiropokwe tuu uliza kwanza kwa wataalamu.
Wazanziabri wanataka nchi yao msijitie visababu vya kipuuzi puuzi.
Acha uvivu wa kufikiri wewe.Wewe ni shaidi kuwa hakuna Mtanganyika wa kawaida anayefaidika na huu muungano so acha kutoa mapovu kushutumu upande wa bara kuwa tunang'ang'ania muungano.
Ungekuwa unamawazo yenye busara nyie upande wa Zenj mkesisitiza muungano.Mnaopinga muungano ni kikundi cha wachache wenye uchu wa madaraka.
Hilo la kufuta UAMSHO ni ndoto za CCM ambazo tafsiri yake ni kukaribisha mgogoro mwengine usioweza kusuluhishika.
Vuai kaona tonge hio inamtoka ndio maana anajikaza kisabuni.
Katiak Uislam huwezi kutenganisha Dini na Siasa kwa7bu siasa ni kajisehemu kadogo ktk Dini ya kiislam ambayo ni mfumo kamili wa maisha wa mwanadamu.
Sasa wewe unaposema nisichanganye Dini na Siasa naona unataka kuniambia nifuate uislam wangu nusu na robo na robo nyengine niiyachie ambayo ndio hiyo siasa, hilo alikubaliki hata kidogo, mwache huyo Vuai na ujinga wake maana hata huo Uislam wake haujui, ndio maana hajui maana ya Dini (Uislam) wala hiyo maana ya siasa yupo yupo tuu !!!!!
Mh Jussa ndiye kiongozi na mfadhiri wa uamsho
Nani alokwambia kwamba Muungano mwisho wake ulikuwa mwaka 1974 kama sii tungo za uongo na Unafiki wa hawa hawa watu wanaodai kuutumia Uislaam iiihali wapo radhi kuongopa kwa faida zao binafsi.Huwezi kufananisha muungano huo na huu feki hata kama unaona kwako wewe uko sawa lakini kwa wataalam kam J. Ulimwengu huu si muungano ila ni muumizano. Muungano ulikuwa mwisho ni 1974 lakini Nyerere (LTLLAH) alipoona Karume anataka nchi yake alimmaliza kwa kumuua kwa risasi na mwaka 1977 alinza kuhodhi kila kitu cha Z'bar. Napia Aboud Jumbe alipojaribu kujitutumua kutaka kujitoa ktk muungano alivuliwa uanachama na kumvua uraisi na kumfunga kifungo cha ndani mpaka amezeeka, alafu unasema muungano huu ni sawa na wa Canada hapo umepotea kaka tafuta ukweli usiropokwe tuu uliza kwanza kwa wataalamu.
Wazanziabri wanataka nchi yao msijitie visababu vya kipuuzi puuzi.
Kwakero zilomo haziwezi kusulihishwa kutokana na wingi wake ukaidi wa Watanganyika kujifanya mabwana wakubwa dhidi ya Wazanzibari, kwa hio kwa hapa tulipofika hakuna mjadala isipokuwa kura ya maoni iitishwe kwa Wazanzibari eidha kuukubali au kuukataa huu muungano, wacheni kunga'nga'nia Zanzibar kwa kisingizio cha cjui usalama, undugu, uasili na mambo mengine yasiyo na mantiki yyte.
Kama ni undugu nadhani pia tumo wengine asili yetu ni Mombasa Kenya, Somalia, Msumbiji Oman, Yemen, Iran, India< China, Comoro etc lakini hatujaungana nchi hizo, na hao wenye asili ya Tanganyika tunao hapa Zenji na waomba mungu uvunjike muungano wawe huru huku Zenji kwani huku ni kwao kama watu wengine.
Iwapo wazanzibari hawautaki muungano mbona dawa ni ndogo tu!!! Hivi ndio kusema Wanzanzibari hawana habari kwamba kati ya vyama vyote vya siasa ni Chadema tu ndio walio na sera za kutaka wazanzibari wenyewe wajadili aina ya muungano wanaoutaka?? Hivi hawa ndugu zetu waislamu wanaliona hilo? Mbona hata punguani anajua muungano ni wa ccm na cuf kwa maslahi ya wachache? Kazi ndogo sana hapo!! Vurugu za nini? Ipeni kura Chadema kupambazuke!!