CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yataka Uamsho Zanzibar ifutwe; Yataka Waziri wa Sheria ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 30, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Chama cha Mapinduzi kimetoa shinikizo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumtaka Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abubakar Khamis Bakar ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kuishauri vizuri Serikali katika suala la kudhibiti asasi za kiraia ikiwemo kikundi cha "Uamsho". Aidha, Chama Cha Mapinduzi kimetaka kufutwa mara moja kwa Jumuiya ya "Uamsho" kwa sababu imekwenda kinyume na malengo yake ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambayo kazi yake kutoa elimu kuhusu mihadhara ya Dini ya Kiislamu tu.

  Akizungumza na waandishi wa habari hapo makao makuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema leo, kuwa kikundi cha kutoa mihadhara ya Dini ya Kiislamu cha "Uamsho" kimesajiliwa kwa ajili ya kutoa mihadhara ya mambo ya dini tu na sio kujishungulisha na siasa za majukwaa, ikiwemo kuwahoji wananchi kuhusu uhalali wa Muungano wa Tanzania na kuwakashifu viongozi wa Serikali, wakiwemo Waasisi wa Taifa hili.

  Alisema kitendo cha Waziri wa Katiba na Sheria kushindwa kuishauri vizuri Serikali kuhusu mwenendo wa kikundi hicho, ndiyo kimesababisha maafa makubwa na kuiingiza nchi katika wasiwasi mkubwa kiasi kuvurugika kwa sekta ya biashara na utalii, "Chama Cha Mapinduzi, kinamtaka Waziri wa Sheria na Katiba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kujiuzulu mara moja kwa sababu ameshindwa kumshauri vizuri Rais pamoja na Serikali kuhusu mwenendo wa kikundi cha "Uamsho" ambacho kinafahamika kwamba kazi yake kutoa mihadhara ya kidini tu na siyo siasa," alisema Vuai.

  Akifafanua zaidi Vuai alisema, kwa mfano, vyama vya hiari vyote vilivyopata usajili wa kudumu wa kufanya shunguli zao vinasajiliwa katika Ofisi ya Katiba na Sheria ambayo ipo katika Wizara yake. Aidha, alisema Mawaziri wa Sserikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walikutana pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa "Uamsho" tarehe 25 Aprili na kutaka kikundi hicho kuacha kufanya mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa au kitachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

  Kwa mfano, alisema hivi karibuni Jeshi la Polisi lilizuia utoaji wa vibali kwa Viongozi wa chama hicho, lakini vibali vilitolewa katika Ofisi za Mufti ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, "Tulimtaka Waziri wa Katiba kulifanyia kazi suala hilo kuona kwamba kikundi hicho hakifanyi mihadhara inayohusiana na mambo ya siasa ikiwemo kuwakashifu viongozi na kuhoji uhalali wa Muungano, lakini hakufanya kazi hiyo," alisema Vuai.

  Vuai alisema, hivi sasa Chama Cha Mapinduzi kimetambua na kufahamu kwamba Jumuiya ya "Uamsho" ipo katika kivuli cha chama kimoja cha siasa na ndiyo maana kimekuwa kikifanya kiburi na jeuri kiasi ya kutamka kwamba hakuna mtu wa kukifuta.

  Aidha, Vuai alisisitiza na kuitaka Serikali kuifuta Taasisi ya "Uamsho" mara moja kwa sababu imekwenda kinyume na dhamira yake ya kuanzishwa, "Tunaitaka Serikali kuifuta mara moja Taasisi ya "Uamsho" kwa sababu imekwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo," alisema Vuai.

  Aidha, Vuai aliwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa watulivu katika kipindi chote na kuacha kujishungulisha na vurugu hizo ambazo zinahatarisha amani na utulivu. Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya "Uamsho", Taasisi hiyo itakuwa na kazi ya kutoa mihadhara ya kidini kwa waumini na wafuasi wake na kulinda haki za binaadamu kwa makundi ya Waislamu mbalimbali.

  Aidha, Jumuiya hiyo kazi yake ni kusaidia kutatua matatizo ya kijamii, ikiwemo migogoro na majanga mbalimbali yakiwemo waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Katiba ya chama hicho inapiga marufuku Taasisi hiyo kujishungulisha na mambo ya kisiasa, ikiwemo viongozi wake.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  taarifa hii imeandikwa na chadema ikasainiwa na ccm tu. Ndio maana magazeti ya uhuru na tanzaniadaima wakatoa picha za ovyo
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna CCM ngapi humu nchini?
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nyerere amejibu mapigo ya Sultani
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Picha gani? Huwa sisomi hayo magazeti.
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kifutwe kimekiuka katiba yake. lakini nimekumbuka kitu hapa hata CCM yenyewe haijasajiliwa kwa msajili wa vyama vya siasa hivyo CCM nayo inatakiwa kutojishugulisha na siasa.
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mapigano ya waislam na wakiristo mto wa MBU jimboni kwa lowasa. kwa hamasa zao za kidini wakaweka mbele kwenye magazeti yao mkuu
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwananchi akipata kichapo kutoka kwa jeshi la polisi baada ya kupita katika njia ambayo zimefungwa na polisi maeneo ya barabara ya Amani na Magomeni Zanzibar
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya ndio majibu yanayotakiwa kutoka kwa kiongozi Mzanzibar ambaye ni mjumbe wa baraza la Mapinduzi, na sii kuendelea kutukashifu kana kwamba sisi Wabara hatumtegemei Allah ktk matatizo yetu. Kusema kweli serikali lazima iwe makini sana na haya makundi ya hizi jumuiya za madhehebu ya dini yanayojitokeza kuchochea serikali za ubaguzi na hata kuzikosoa imani za dini kwa matakwa ya tafsiri zao wenyewe.
   
 10. R

  RMA JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi nazo ni porojo tu! CCM walitumia Green Guard wakaona haifai! Wakatumia Bakwata, wakaona hailipi! Sasa wanajificha chini ya mwavuli wa Uamsho, lakini bado wamegundulika!

   
 11. F

  FUNGO jr JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  heshima kwako mkuu
   
 12. R

  RMA JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iwapo wazanzibari hawautaki muungano mbona dawa ni ndogo tu!!! Hivi ndio kusema Wanzanzibari hawana habari kwamba kati ya vyama vyote vya siasa ni Chadema tu ndio walio na sera za kutaka wazanzibari wenyewe wajadili aina ya muungano wanaoutaka?? Hivi hawa ndugu zetu waislamu wanaliona hilo? Mbona hata punguani anajua muungano ni wa ccm na cuf kwa maslahi ya wachache? Kazi ndogo sana hapo!! Vurugu za nini? Ipeni kura Chadema kupambazuke!!
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kumlazimisha waziri kujiuzulu na kuamuru jumuiya ya uamshi ifutwe ndio solution ya tatizo?
   
 14. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio mgogoro utakapoanza, kwa ufahamu wangu mimi, DINI ni mfumo kamili wa maisha na Siasa ni just kisehemu ndogo tu chahiyo dini.

  Huu ni mgogoro mwengine, wizara hii ipo chini ya CUF, na CCM wanatoa shinikizo waziri wa CUF afute kikundi hiki.

  Hapa patamu sana, wait and see
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mnaacha kuangalia mzizi wa tatizo, mnatafuta simple and cheap solution.

  Wakati wa rasimu ya katiba tuliona yaliyomtokea sitta, na wala haikuwa uamsho, vikundi vya jamii mbali mbali vilialikwa rasmi, lakini ukitazama zile video kila aliyesimama aliongea kwa jazba na mwisho ni kuukataa muungano tena kwa hasira, Kuna mwanajeshi mstaafu alilia.

  Busara zinahitajika sana naamini, sio kufuta usajili.
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ndoa ya CCM na CUF ipo mashakani?
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa sina habari kumbe Mufti anaweza kutoa kibali cha maandamano.
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ndo maana wanataka nchi yao.
  System yao tofauti.
   
 19. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vuai umenena vyema ingawa tayari umesha chelewa kwani tangu mwanzo malengo ya kikundi hiki yalikuwa ya kisiasa zaidi
   
 20. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,802
  Likes Received: 2,575
  Trophy Points: 280
  Ha ha hii kitu inaitwa pragmatism, mkono mmoja piga kura, mwengine ziba pua!
   
Loading...