CCM si wajinga tusiwa underestimate. kwanza tutambue Usalama wa taifa (Uhasama kwa taifa), Polisi (Policcm), Spika wa bunge, Wakurugenzi, Wakuu wa jeshi, wote hao kwa umoja wao (namaanisha wengi wao ni mafisadi) wanakaa na kupanga. Pia tusisahau propaganda machine ambazo ni CloudsFM, TBC na magazeti ya serikali. Pia Msajili wa Vyama, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mkuu. Hawa ni watu wenye dhamana kubwa na nyadhifa nyeti.
Bado hatupo salama, tena tuko kwenye vita kubwa kuliko wakati mwingine wowote kwani adui yetu anafahamu fika nguvu yetu kuwa ni Umma, wananchi wanyonge waliodhulumiwa haki zao. Hivyo basi tusidhani maadui hao watalala usiku kwa raha mpaka wahakikishe wametuangamiza kwa hila zao chafu. Hili la Lwakatare ni mwanzo tu, mengi yanakuja.
Tufanye nini?
Yatupasa kuongeza mapambano yetu kwaq kuzidisha M4C ili elimu ya uraia na kiu ya ukombozi izidi kuenea hususan maeneo ambayo bado ni ngome ya mafisadi kama vile Dodoma, Moro, n.k
Kila mwana cdm kwa nafasi yake ahakikishe anatoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi kadhaa uswahilini ambao bado hawafahamu umuhimu wa kupiga kura na thamani ya kura, hususani vijana wenzetu ili wasiishie ushabiki tu bali wawe wapiga kura. Hapo ndipo tutaweza kupambana na majuha yanayofilisi mali za nchi hii