Ccm wapata ajali pemba

pembankwetu

Senior Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
133
Reaction score
62
Makada 14 wa CCM wajeruhiwa ajalini
Na Hamad Shapandu, Pemba
MAKADA 14 wa CCM wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Micheweni kwenda Konde kisiwani Pemba,kupoteza mwelekeo na kugonga mti.

Gari hilo aina ya Minibus yenye namba za usajili Z505 BQ iliyokuwa ikiendeshwa na Humud Seif Humud ilipata hitilafu hiyo muda mfupi baada ya kuondoka kituo cha magari Micheweni ikiwa imebeba wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, wilaya ya Micheweni.

Mganga wa hospitali ya Micheweni, Dk. Amour Suleiman Khamis alisema majeruhi wote 14 walifikishwa katika hospitali hio na baadhi yao walikuwa wameumia vibaya.

Alisema abiria 10 walitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani, huku wengine wakiendelea na matibabu.

Aliwataja walioumia kuwa ni Salimu Busaga Dida mkaazi wa Makangale, Halima Abeid wa Msuka, Omar Hamad Sheha, Khamis Juma Faki wa Konde, Msellem Kombo, Abdi Said na Amina Khatib Ali wa Msuka.

Wengine ni Riami Khamis Shaame, Ramadhan Omar Ahmed, Hadia Khamis Juma wote wakaazi wa Konde, Juma Omar Khamis wa Kifundi, Muhammad Ali wa Kicha, Kidawa Suleiman Khatib na dereva wa gari hilo, Humud Seif.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis walikuwa miongoni mwa viongozi waliokwenda kuwafariji majeruhi hao na kuwataka wawe na subira katika wakati huu mgumu.

Majeruhi Riami Khamis Shaame na Ramadhan Omar Ahmed walisema gari hilo halikuwa na mwendo wa kasi bali hitilafu za kufunguka ‘tairod’ ndio chanzo cha ajali hiyo.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa hususan viongozi wa CCM, wafanyakazi na wananchi wanaendelea kuwajulia hali katika hospitali waliyolazwa.
 
Chama kile kile chenye kufurahia vifo ili kuongeza umaarufu wao kisiasa.

Na kwa vyovyote CHADEMA wanhusika kwani wanatafuta umaarufu wa kisiasa kwenye Vifo na Hasa Lema bila Kusahahu Mbowe , Shime Chagonja kamata hawa viongozi kwa kusababisha ajali Pemba.

Akili Ndogo Vs Akili Kubwa.
 
Chama kile kile chenye kufurahia vifo ili kuongeza umaarufu wao kisiasa.

Tulia we mliberali, kama mnaona vifo vya watu vinatupa umaarufu basi acheni kuwaua. Kwani mlipomuua Mwangosi mlidhani kuku yule?
 
Kama wako hai hiyo ni habari mbaaya sana nilitegemea uniambie wote wamekufa kibudu manyang'au hayo sipendi kusikia habari zao njema maana yanaua watu wasio na hatia kwa kutafuta umaarufu ambao hata hivyo unazidi kupotea
 
Israeli nae bwana!! Kwa nini hakuya chukua haya majamaa? Mi nilikuwa najua yamesha kata pumzi kumbe bado!!!
 
Tuliko fika n kubaya! Yaani ukiwa mwanachama wa ccm watu wanatamani ufe!
 
JF inabariki watanzania Wachukiane kwa kiasi hiki! God where are we heading?????
 
JF inabariki watanzania Wachukiane kwa kiasi hiki! God where are we heading?????

Kazi ua jamiiforums ni kuwakilisha habari kwa jamii husika,hizi unazoziona humu ni hasira za watu dhidi ya utawala wa kifisadi.
 
JF inabariki watanzania Wachukiane kwa kiasi hiki! God where are we heading?????

acha uliberali JF ndo wanaandika au hayo ndo yaliyopo katika mioyo ya watu? Wakikusanyika katika mikutano mnawapiga mabom na risasi acha wabwage mioyo yao humu, JF hakuna mabom wala risasi hapa ni fair ground.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…