CCM wanaliweza hili?

Joss

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
765
Reaction score
192
Tumeshuhudia wakati mwingine CCM kutokufanya usawa katika miradi ya maendeleo hasa katika maeneo walipopata kura chache au walipochagua upinzani,mf. madiwani katika jimbo la Chato kwa Magufuli wamekuwa wakilalamika uonevu huu na kauli chafu za mbunge huyo kwa wananchi wao kuwa wasahau maendeleo kwa kuwa wamechagua upinzani...

Soma jinsi Nassar anavyoanza kufanya kazi yake,...

katika kuanza kutekeleza shughuli za kimaendeleo Nassari alisema

"Naomba mnitie moyo na kuna kata nimeshinda na kuna kata nimeshindwa, lakini kwa kuonyesha upendo nitaanza na kata walizonipa kura chache, lakini nashukuru sana leo mmetuma salama kuwa hata mtoto wa maskini anaweza kuwa kiongozi," alisema.
"
 
Inaonekana Pande zile kuna ubaguzi mkubwa sana wa kiuchumi.
 
Big up nassari endelea kuwatumikia wanaarumeru bila ubaguzi na mungu atakujazia
 
Hekima ndogo huota kama uyoga na kuwa kubwa, endelea kamanda nassari
 
kijana mdogo busara nyingi na nguvu daima, mtenda kazi,fanyakazi ndo shukurani kwa wapiga kura wako na jimbo lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…