MkamaP,Watanzania tuna tatizo .
japo wengi wanajaribu kurusha mpira kwa watu wa kijijini ,eti waelimishwe kweli mie mtoto wa kijijini nafadhaishwa sana na kauli za namna hii.
Nakubali ,kweli na hakika ni tabia ya binadamu asiye mwelevu(yani mpumbafu) akifikiri yeye ni mwelevu. Binadmu huyu ana tabia ya kuhamisha tatizo ya kwamba lazima tatizo hili nililonalo limesababishwa na fulani na wala si yeye.
fuatilia tu, binadamu mpumbafu hata kama akiwa amebeba bilauli yake ya maji na bahati mbaya akaidondosha na kupasuka ,binadamu mpumbafu lazima atatafuta wa kumtushwa tatizo hilo.mfano mbona umeweka kiti hapa, ama kitambaa hiki ndo kimesababisha .
binadamu mpumafu siko zote hatafuti chanzo cha tatizo, na mara zote atatafuta jibu jepesi kabisa nalo ni kumtwika hilo zigo mtu fulani.
Jamani nawaombeni kwa niaba ya wanakijiji wenzagu ,mtupe kalikizoeti ya kwamba mnataka kutuelimisha,eti ya kwamba sisi ndo chanzo cha matatizo,eti ya kwamba sisi ndo tunaiweka ccm madarakani.
One moment
Lakini nikijaribu kufunua na kuperuzi kumbukukumbu na wanakijiji wenzagu naona kumbukukumbu zinaleta takwimu ya kwamba sisi wavijijini, tusio na elimu tuna historia nzuri ya kupeleka wabunge wa upinzani bungeni ,tofauti na wasomi na watu wa mjini .
Ehe
Sisi wanakijiji tunachojiuliza je tatizo la tanzania ni sisi wanakijiji,tusio na elimu? ama tatizo ni wamjini na wasomi ?
kwanini sisi wa vijijini tunabebeshwa mizigo? je ni kwa sababu hatuna media kama jamiiforums.com ama ITV?
Je tatizo lina mizizi yake i mingine tofauti ila kwa sababu ya upumbafu wa watanzania wote hasa wasomi na wamjini wanajaribu kutafuta jawabu rahisi kuhalalisha upumbafu wao.?
Pasco hilo la Sitta kutoka nje ni la kweli kuna gazeti moja la hapa Tanzania nadhani ni Mwanachi limeripoti kuwa Sitta, Anna Kilango, Dr Mwakyembe walitoka nje na wakaingia kwenye ofisi moja na humo walikaa zaidi ya saa moja na nusu wakijijadiliana na badaye walirudi kwa nyakati tofauti akianza Mwakyembe, baadaye Kilango na mwisho Sitta.
Mimi hawa jamaa wa 16 na mwenzake Kileo naamini sehemu kubwa waliyokuwa wakiongea ni ya UKWELI ila sijui wanaongea kwa maslahi ya nani! Saa nyingine huwa najiuliza hawa jamaa wanaoshinikiza akina wa 16 walete vitu ni kweli wanavitaka hivyo vitu au 'kimtindo' hawavitaki na wanachofanya ni vitisho vya 'kimtindo??
JF!!!! I dare to listen!!!
Angalia sana haya magazeti ya Bongo mengi siku hizi yanatumia JF kama chanzo cha habari
Hiyo ya kutoka nje kwa hao unaowasema ili ripotiwa jana J3 na magazeti na walitoka nje siku ya Jumapili siku ya kwanza ya kikao cha NEC si jana J3 wakati hiyo thread ya kilewo ni ya jana J3 acheni fix zenu hata hivyo hatuhitaji tena audio yake tumeshapata ajenda zake
Luteni,
Hata kama hukubaliani na kinachosemwa lugha za kibabe hapa sio mahali pake! Ushafahamu! Hata sisi twazijua. Kwani Kilewo alitaja Sitta alitoka ndani lini? Au kwa sababu aliongea j3 na kwa hiyo lazima Sitta alitoka ndani j3 na si j2? Kama tunavyokusikiliza wewe ni haki yako na mtu mwengine yoyote ana haki ya kusikilizwa. Sasa kama wewe umeshapata hizo ajenda mbona hujatuletea hapa?? Nina imani Uluteni wako ni wa 'kiukweli' na si kama wa kina Makamba!!
Luteni,
Hata kama hukubaliani na kinachosemwa lugha za kibabe hapa sio mahali pake! Ushafahamu! Hata sisi twazijua. Kwani Kilewo alitaja Sitta alitoka ndani lini? Au kwa sababu aliongea j3 na kwa hiyo lazima Sitta alitoka ndani j3 na si j2? Kama tunavyokusikiliza wewe ni haki yako na mtu mwengine yoyote ana haki ya kusikilizwa. Sasa kama wewe umeshapata hizo ajenda mbona hujatuletea hapa?? Nina imani Uluteni wako ni wa 'kiukweli' na si kama wa kina Makamba!!
Mkuu Pasco,.
Alibaba, asante kutujulisha, kumbe sasa angalau mnalala?. Basi nitamweleza Invi na wanabodi wengine na sisi to relax.
Asante pia kujitambulisha kwa kutupatia hakikisho la habari yenye uhakika asilimia 99% ili kutuonyesha wewe ndio namba 2 chini ya Othman, maana kama hata huyo namba 3 hawezi kuwa na uhakika na namba 2.
Tumekusikia kumbe hizi ni kelele tuu za mlango... ngoja nasi tujilalie, kumbe wenyewe wamelala na hawakosi usingizi!.
Angalizo kwako Alibaba, usijekuta kumbe wewe ndio mfungua geti hapo nje, hivyo wala hujui mle ndani kinaendelea nini, ukishaona tuu wamezima taa na kufunga ofisi, basi umejiridhisha wemeshafunga kazi, hivyo wamekwenda kulala, na wewe unajifungia zako geti ukiwasubiri asubuhi waje kazini, asubuhi ikifika unawafungulia geti ukiamini ndio wametoka kuamka na ndio wanaingia kazini!, na wewe ndio unatoka shifti na kwenda kujilalia!.
Asante kwa taarifa hizi!.
Kenge,Thread hii bomu, JF sio sehemu ya uzushi. Kama huna taarifa kaa kimya sio kutunga na kupotezana kifikira CCM NEC hawajadili haya yanayoongelewa hapa.
ANGALIZO.