CCM ni mkoloni mzawa

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
326
Reaction score
67
Ingawa siyo mtaalam wa historia lakini nakumbuka kidogo kwamba wakoloni walipotutawala walitaka tuamini kwamba bila wao sisi tusingeweza kujitawala huku wakifanya tafiti mbalimbali za madini na kuiba maliasili zetu hadi tulipojitawala. Hakuna mkoloni aliyependa kuachia nchi ijitawale bali walijaribu kutudunisha na kuuaminisha umma kuwa kila aliyetaka tujitawale ni gaidi, mhaini au lugha nyingine yeyote iliyowapendeza wao.

Kule Afrika ya kusini wakati mmoja kaburu Peter Botha alidiriki kutamka kuwa, nanukuu: 'pamoja na kwamba waafrika wanafanana na binadamu kama sisi (yaani kama wao wazungu) haina maana kuwa wanakamilika kuwa binadamu kamili', mwisho wa kunukuu. kauli Kama hiyo si njema na ingeweza kuwakatisha tamaa waafrika lakini walikaza kamba......wakauawa, wakateswa, wakafungwa gerezani na kudhalilishwa kana kwamba kweli si binadamu. Mwisho leo S.Africa wako huru na mzungu chini ya rais mwafrika.

Ndugu zangu wa chadema, hatua tunayoipitia ni ya muhimu mno! Kumbuka walianza kuwahonga kina sonza ikashindikana, sasa wanatapatapa lakini mkoloni mkoloni tu! Wanaweza wakaondoka na mtu kikweli wakamfunga ama vyovyote walivyopanga, lakini tuliobaki tukaze kamba kuuelimisha umma juu ya uhalifu wa mafisadi hawa ili 2015 tuwaondoe kwa kura kama alivyoondolewa kaburu wa afrika kusini na mkoloni wa kiingereza nchini mwetu.

Wenzetu wa cuf walijaribu lakini propaganda za mkoloni mzawa (ccm) zikawashinda: mara waambie chama cha kidini, mara magaidi wameingiza masime na igp mahita akautangazia umma kwa njia ya tv na wanachama wengine wa cuf waliuawa na wengine kusota rumande kwa miaka kadhaa. Maalim kuona hivyo akaambiwa wafanye muafaka! Lo! Tusidanganyike. Peopleees power!
 
kama CCM ni Mkoloni - CDM ni kina kina KIBANGA.
 
Wakoloni tunaowasoma kwenye historia wangekuwa wakatili kama walivyo viongozi wa Serikali na CCM naamini kabisa asingebaki mtu mweusi hata mmoja hapa duniani na bara la Afrika lingezamishwa kabla ya karne ya 20.
 
Wakolini walikuwa wanjua namna ya kutawala na sio kama uozo wa CCM na vinogozi wengi wa kiafrika.

On mawazo ya mkoloni yalivyo kuwa.
 

CDM bepari mzawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…