CCM malingalinga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,649
Reaction score
830,488
Malingalinga ni hali ya kuwa hobelahobela, mzobemzobe, bila utaratibu MBELE KWA MBELE
Tuna vitengo viwili vya propaganda hapa jukwaani, kitengo cha propaganda cha UKAWA hawa wanajitolea hawalipwi chochote ni wanamabadiliko, propaganda zao ni za kisera na kimfumo zaidi
Halafu tuna kitengo cha propaganda cha ccm... Hawa ni pasua hasa, wako kwenye payroll wanalipwa kuandika ujinga, hawajadili sera wala mfumo... Bali personal attacks.. Tena za kutunga hasa... Hawana uwezo wa kuandika chocolate bali wameandaliwa kwenye makaratasi nini cha kupost, na ndio maana wakishapost chochote huingia mitini kwakuwa hawana uwezo wa kukitetea walichopost na wakijaribu kufanya hivyo ni upuuzi mkubwa

Hiki ni kipindi cha mabadiliko wananchi wana mwamko wa ajabu wamejitambua, wamejifahamu, wanataka kitu kingine tofauti nje ya mfumo waliouzoea na kuwalemaza kwa miaka 50
CCM lazima walitambue hili, kwahiyo waache propaganda za kipuuzi na zisizo na mashiko kwakuwa baada ya uchaguzi maisha yapo, na dunia inaangalia kwa karibu kabisa LAKINI VILEVILE na Jamii Forums iwe makini isitumike vibaya....iwe makini na hili ongezeko la ghafla la 🆔 ambazo kwa asilimia 95 zinapost habari za viongozi wa UKAWA tena kwa njia ya kukejeli kutukana kukashfu na kuongea uongo na upuuzi wa kila aina
 
ccm haipaswi tena kumshambulia watu, haihitaji kutoa ahadi mpya, hiki ni chama kilichopo madarakani kiwaambie wapiga Kura na wananchi kimetoka wapi kiko wapi na kinakwenda wapi, kilifanya nini kimefanya nini na kitafanya nini, kimefanikiwa wapi na kwanini kimeanguka wapi na kwanini na kinajitathmini vipi kuweza kuaminika tena
Ahadi waachiwe wapinzani hawa hawajawahi kushika Madaraka hivyo ni lazima waahidi
 
Kweli kabisa mkuu

Lakini wenyewe hawawezi kukubali huu ukweli Sanasana ile timu ya propaganda za kipuuzi ndio itajaribu kujitutumua, wale ccm wa lumumba tuliowazoea kuwaona jukwaani 24/7 Sijui wameyeyukia wapi.. Most likely wameretadi na sasa ni wana mabadiliko kwa 🆔 mpya
 
dah payroll ndo inaleta shida,lakini naamini payroll haiwezi kwenda popote
 
dah payroll ndo inaleta shida,lakini naamini payroll haiwezi kwenda popote

Kitanuka baada ya uchaguzi, pale watakaposhikana mashati kuwa ndani yao waligeukana wao kwa wao na wakapiga ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…