Kigongoi kwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2018
- 559
- 661
Ok tumekuelewa! Basi basi oktoba 28 itaamua nani anastahili kutawala nchi hi!
Kwamba, kwa sasa haiwezi kutawala peke yake, mawazo ya pekee kwa sasa hayana nguvu, Kwamba, upinzani umekua na utaendelea kukua na kwamba kutumia njia za kistaarabu ndio njia pekee ya kuienzi amani ya nchi na kwamba elimu ya wananchi kuhusu upinzani imeongezeka.
Kwamba hoja zinapaswa kujibiwa kwa hoja na wala sio kutumia vyombo vya dola kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa chama hicho kwamba wanatumia privileges za dola kubaki madarakani.
Na kwamba kuna haja ya kukaa na upinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya siasa kwa amani bila kuleta mpasuko wa Kitaifa au kuwa na chuki miongoni mwetu.
Nakumbuka Rais mstaafu Kikwete wakati wa awali wa maandalizi ya katiba ya Jaji Warioba alisema,ni bora kukaa pamoja na kujadili yanayotuhusu tukiwa pamoja, kuliko kutafuta umoja tukiwa tumetofautiana.
Nawasilisha
Ukimsikia mtu anaongelea kufuta upinzani, ujue ana shida katika akili yake.
Kwa ustaarabu wa Dunia ya leo ni lazima uwe kichaa kufikiria kuwa unaweza kuongoza huku watu wote wakisema NDIYO MZEE. Ukiona mtu ana mawazo hayo, jua huyo hajitambui wala haitambui Dunia.
Wewe ni nani hata kila mmoja akusikilize wewe tu? Kama ni binadamu kama walivyo binadamu wengine ujue utapingwa, utakosolewa na kuna wakati unaweza hata kukejeliwa. Hayo itayapata tu maana hata ungekuwa Rais, Waziri, Mkuu wa majeshi au IGP au hata mkurugenzi wa wasipjulikana, wewe bado ni binadamu tu. Hujabadilika wala kubadilishwa chochote. Uliochopewa ni wajibu tu wa kipindi kifupi.
Kisichobadilika na hakiwezi kubadilika mpaka siku yako ya kwenda kaburini, ni ubinadamu wako tu. Madaraka, uongozi na vyeo, vinakuja na kutoweka.
Usijivunie cheo au madaraka yao bali jivunie ubianadamu wako. Jiulize umekuwa mwanadamu kwa kiwango gani. Ubinadamu wako ndio unaoweza kukufanya uwe kiongozi wa namna gani.
Kiongozi kuwa dikteta, mbaguzi, mbabe au mwerevu, mwenye upendo, mwenye kuthamini utu wa anaowaongoza, hutegemea zaidi kiongozi huyo ubinadamu wake ni wa kiwango gani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ni changizo bora kabisa katika thread hii na zote za aina hii. Nakubaliana nawe mkuu unaposema HAKI haijarishi nani au chama gani kinaongoza hii nchi yetu na nia ya kweli (spirit of readyness) ya kuikwamua nchi ilipo kusonga mbele katika nyanja zote za maendeleo pasipo ubaguzi wa ukanda bali as Tanzania kwa ujumla wake.Una maono mafupi sana, ndio utaendelea kubaki hapo chini ulipo!! Swala sio kutawala ni kuongoza na ndio point ya mleta mada. Swala ni maelewano, maridhiano, amani, haki na ustawi wa jamii nzima. Kama nchi hatutakiwi kuchagua haki! Haki inapaswa kuwepo bila kujali nani anaisimamia!! Hatutakiwi kuogopa nini kisisemwe! Tunapaswa kushughulika na nini kimesemwa.
Unafahamu zero-sum versus win-win approaches? Nchi hii inamuhitaji kila mmoja wetu kwa nafasi yake katika ustawi wake. Mambo ya kitaifa hatuhitaji kuyabishania, tunapaswa tu kugombea kuyatekeleza!!
Amani yetu imeshikiliwa na wapinzani hichi ni kizazi cha sasa ni dotcom kina exposure. Busara za mbowe na maalimu ndio utulivu wetuKwamba, kwa sasa haiwezi kutawala peke yake, mawazo ya pekee kwa sasa hayana nguvu, Kwamba, upinzani umekua na utaendelea kukua na kwamba kutumia njia za kistaarabu ndio njia pekee ya kuienzi amani ya nchi na kwamba elimu ya wananchi kuhusu upinzani imeongezeka.
Kwamba hoja zinapaswa kujibiwa kwa hoja na wala sio kutumia vyombo vya dola kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa chama hicho kwamba wanatumia privileges za dola kubaki madarakani.
Na kwamba kuna haja ya kukaa na upinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya siasa kwa amani bila kuleta mpasuko wa Kitaifa au kuwa na chuki miongoni mwetu.
Nakumbuka Rais mstaafu Kikwete wakati wa awali wa maandalizi ya katiba ya Jaji Warioba alisema,ni bora kukaa pamoja na kujadili yanayotuhusu tukiwa pamoja, kuliko kutafuta umoja tukiwa tumetofautiana.
Nawasilisha