Maana chama chenyewe ni mchafu kunuka kwa kila aina ya uchafu unaowahitaji Watanzania wakiweke kando.
CCM iko kwenye wakati mgumu sana like no any other time in history. Hadi wanafikiria kuiingiza nchi kwenye machafuko kwa kuahirisha uchaguzi ili eti wajipange kuweza kushinda!
CCM imepoteza uhalali wa kisiasa Kwa muda mrefu na sasa inaanza kujipotezea hata uhalali wa kisheria.
Kumbe hujui, chuma kikipita kwenye moto huwa laini ile mbaya, ndio maana wahunzi huambiwa kukigonga chuma kingali moto!Chuma kikipita kwenye moto huwa imara zaidi...
Kumbe hujui, chuma kikipita kwenye moto huwa laini ile mbaya, ndio maana wahunzi huambiwa kukigonga chuma kingali moto!
ni lazima ccm wajipange hasa kwa ngazi ya urais
Swala sio faraja, unapoandika ujue unakusudia kupeleka ujumbe gani. Tatizo la ma CCM mnadhani kila mtu ni mbumbumbu kama ninyi mlivyo!Mnajua kujifariji...
Mambo hayaendí. Vituko,mwitiko na mtikisiko umetamalaki. Kwanza,Katiba mpya imegoma. Hakika,katiba mpya ingekuwa chapuo muhimu kwa CCM katika kampeni za mwaka huu-kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba. Pili,UKAWA wanavyokaa kimya kumtaja mgombea wao wa Urais ni pigo kwa CCM. Chama kilijipanga kumshambulia na kumsawajisha mgombea wa UKAWA na ndipo wetu angetangazwa. Ukimya wa UKAWA ni kuminywa kwa CCM.
Tatu,CCM kila uchao inapiga mahesabu ya nani awe mgombea wa Urais. Awe mwenye kashfa au sifa? Awe mwenye mvuto au uvundo? Awe toka Serikalini kulikoandamwa na kila rangi ya rushwa au toka nje ya Serikali ya awamu ya nne? Hali tete.
Nne,kashfa za ufisadi ni doa kuu kuelekea Oktoba. Pamoja na Serikali kuwasafisha watuhumiwa,mbele ya wananchi watuhumiwa hao ni wachafu na wasiofaa. Mbaya zaidi,watuhumiwa hao ndio wenye nguvu hata ya kupenya kwenye Urais. Kashfa za kifisadi zinazotajwa ni pamoja na Richmond,EPA na Escrow. Wananchi wanazikumbuka na wanawakumbuka watuhumiwa.
Tumaini la CCM yetu ni NEC ya Jaji Damian Lubuva. NEC inategemewa kufanya mambo ili uchaguzi wa Oktoba uote mbawa. CCM ipate muda wa kujipanga. Ipate ushindi. Lakini,hakuna dalili za NEC kuiponya au kuipunguzia maumivu CCM. Itapambana hivyohivyo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Swala sio faraja, unapoandika ujue unakusudia kupeleka ujumbe gani. Tatizo la ma CCM mnadhani kila mtu ni mbumbumbu kama ninyi mlivyo!
Achana na lugha za mateja hizo! Unapoandika uwe na malengo na sio kukurupuka. Taabu ya nyie wahitimu wa shule za kata ni kwamba hamkufundishwa jinsi ya kujenga hoja makini na ndio maana mnaishia na vijineno vya kwenye kanga!Mtarukaruka kama bisi ila mwisho mnaishia kutafunwa...