Kwani wanaelewaga sasa, ukishakua na wabunge kama msukuma, nchi itaenda sasa?Wabunge wa CCM wanatumia vibaya Bunge kuanzisha mgogoro wa kidiplomasia na Kenya bila sababu za msingi. Kauli zao ni za kiholela, hazizingatii athari za kiuchumi wala kijamii, na zinaweza kuumiza raia wa kawaida wanaofanya biashara au kuishi pande zote mbili.
Maneno ya chuki dhidi ya raia wa Kenya si tu yanaweza kurudishwa kwa Watanzania walioko Kenya, bali pia yanahatarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili. Kenya ni mshirika mkubwa wa biashara, utalii na uwekezaji kwetu. Takwimu za kibiashara na utalii zinaonyesha ushirikiano huu ni wa manufaa kwa pande zote.
Badala ya kulinda maslahi ya taifa, wabunge hawa wanachochea chuki kwa misingi ya siasa za mitandaoni. Huu ni ushamba wa kisiasa na ukosefu wa dira. CCM mmeshaua mambo mengi ndani ya nchi, msije sasa mkaharibu mahusiano ya kimataifa. TUNAHITAJIANA.
Namna ipo, labda wizi wa kura ushamirishwe.Hawatakuelewa,
Nionavyo mimi na tafukuri yangu, katika nchi wanachama wa jumuia ya afrika mashariki tz na kenya ndio wenye nguvu sana, narudia tena, nionavyo mimi. Sasa kwa mwendo wa kuchangia kwa ajili ya kumfurahisha malaika, umoja huu siku zake zinahesababa na zinahesabika kutokana na ushabiki tu wa kushindwa kujenga hoja,
Namshukuru yule mbunge aliyesema tusizichape ng'ombe kwa sababu tunaharibu radha ya nyama, nyinyi ndio wabunge wetu hatuna namna