Ccm bwana!!

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,665
Habari za jioni?
Wakuu tuache utani ama chuki binafsi, CCMni chama kinachoona mbali.......Kwa nini????
Sonsomokahapa...


  • Kwamba imeona wananchi wake wanavyonyanyasika asubuhi na jioni wakati wanataka kwenda makazini ama kurudi nyumbani. Utakuta daladala inaona kabisa watu wamesubiri basi hilo lakini anakataa kusimama palepale walipo abiria….anakwenda kusimama mbali ili aone jinsi raia wanavyokimbilia basi hilo yeye roho yake kwatu……’. Ndipo CCM ikaona ni vema serikali yake itatue tatizo hilo kwa kuweka mabasi yaendayo kasi. Hapo hakuna kukimbilia basi! Litakuwa linasimama miguuni!!!


  • Kwamba taabu za kulipa marambili eti kwa kuwa unakwenda mbele kugeuza na basi hilo unatozwa nauli mara mbili japo umegeuza palepale. Unatangaziwa basi linakwenda makumbusho hivyo unalipa mara mbili lakini lageuza palepale kurudi mjini. Manyanyaso makubwa sana! Lakini sasa mabasi yaendayo kasi itakuwa hakuna kulipa mara mbili maana hata kugeuzia njiani miundo mbinu hairuhusu.



  • Kwamba ilikuwa asubuhi ukiamka (mpaka sasa) unakwenda kituoni kupanda basi la kwenda kazini ama nyumbani bila kuwaa na ratiba. Yaani haijulikani basi litakuja saa ngapi. Ilikuwa ni masuala ya kubahatisha. Lakini sasa ratiba itawekwa na mabasi yaendayo kasi yatakuwa yanatunza muda


WATU KULAUMU CCM KWAKILA JAMBO….
Kutokana na madhila yooote wanayoyapata wananchi (kama haya ya kunyanyasika na madaladala) watu hutupalawama zao kwa CCM. Tuwe wakweli!!! Kwa abiria kunyanyaswa kamanilivyoeleza hapo awali je nani ni mtu wa kulaumiwa wa kwanza? Kama ni lawama sisi raia wenyewe (in this sense-wamilikina wahudumu wa daladala!). Unapoilaumu CCM wakati wewe ndo mtu wa kwanzakuvunja sheria mimi kama msomi sikuelewikabisa! Inatakiwa raia uwe mstari wa mbele katika kutenda haki ili serikaliitakapozembea katika utekelezaji wa (mfano) kusimamia sheria uzembe huo huwawazi kabisa. Abiria umnyanyase wewe kwa kukosa uzalendo na ubinadamu lakinilawama umtupie CCM……..! Hii siyo sawa.

Raia unatakiwa kuwa mwadilifu kwanza kisha vyombo vyadola ndo vifuate. Hii itaondoa lawama za kulaumu ulipoangukia badala ya kulaumuulipojikwaa.




JE CCM IMETHIBITISHA KUWAJALI WANANCHI WAKE?
Jibu ni ndio…..Hebu cheki vituo vya mabasi yaendayo kasi…….Rangiiliyopakwa ni ushahidi kwamba kazi hiyo nzuri ni juhudi za CCM! (Ingawa watuwenye “alergy” na CCM wataachakupanda mabasi yaendayo kasi kwa kuwa yana rangi ya CCM) lakini nataka niwaasewasifanye hivyo…..Hata wao wamenyanyasika na wanaendelea kunyanyasika nawamiliki na wahudumu wa mabasi wasiojali utu….Pesa kwao mbele kuliko utu…….Nawaombeni mradi utakapokamilika wapande mabasihayo kwa wingi maana itawapunguzia gharama za kulipa mabasi matano mpaka mananekwa siku. Pia haitakuwa na haja ya kumiliki gari kamamatumizi yake makubwa ni kumfikisha mtu kazini na kurudi tu.

Kwa kuniunga mkono nawaombeni wenye picha current yavituo vya mabasi vilivyokamilika na vinavyoendelea kujengwa wazitundike humu.


Asante sana!
 
CCM noma, uwanja wa Ally Hasani Mwinyi Tabora wameugeuza shule ya chekechea. Vyumba vya kupumzikia timu; kimoja darasa, kingine jiko la kupikia uji wa watoto hao.
 
CCM noma, uwanja wa Ally Hasani Mwinyi Tabora wameugeuza shule ya chekechea. Vyumba vya kupumzikia timu; kimoja darasa, kingine jiko la kupikia uji wa watoto hao.

Anzisha thread yako itakayozungumzia hilo. Usichomeke hoja nje ya kilichopo. Nasema hivyo nina sababu nzuri.
 
Anzisha thread yako itakayozungumzia hilo. Usichomeke hoja nje ya kilichopo. Nasema hivyo nina sababu nzuri.
Wewe ulichofanya ni sawa na kupulizia maiti pafyum, lkn fahamu huwezi zuia harufu
 
Mabasi ya endayo kasi hayatakuwa suluhisho la foleni ndefu katika jiji la darisalama. Wanafikiri kuwa kinacho sababusha foleni ni magari mengi, si kweli. Foleni zinasababishwa na miundo mbinu hovyo na yakizamani. Mfano, jinsi barabara ya morogoro ilivyo pana pawe na laini nne kwenda na nne kurudi , kwenye viunganishi vya barabara taa za kuongozea magari ziondolewe na pawekwe njia Za juu. Ni ajabu kuwa na viunganishi barabara vye kuongoZwa na taa kwenye high way kama ya morogoro road. Tukifanya huvi tutaondia foleni
 

Pamoja na maneno yako mazuri na yenye ukweli lakin uko nje ya mada mkuu.....mada ni kunyanyasika na mabasi ya daladala....hebu soma vizuri mada kasha utanielewa.
 
maccm ni mashetani tu watz tumewachoka hata mtuletee helcopter swala liko palepale hamtakowi, juzi mlikuja Arusha kupima kina cha maji baada ya kumchafua lema muone baada ya ujinga wenu mliofanya je lema hakubaliki? aaah wapi mkaambulia watu 20 mawakala wa shetani nyie hyo mabasi naamini watu tukfatilia tutakuta kuna mlungura wa kufa mtu si ndo dili zenu nyie
 
Kumbe hauna data. Mabasi yaendayo kasi mradi tuliambiwa una pesa na utakamilika 2009, kwa serikali ya CCM pesa ikaliwa na hadi leo mradi hauna dalili ya kutimia miaka hii ya karibuni. Sifia tu CCM lakini sisi wananchi tumekosa imani nayo tunasubiri ifike 2015 tu
 

Mbona uko nje ya mada? Mada ni kunyanyasika kwenye mabasi ya daladala! Au wewe hunyanyasiki? Na ukombozi wa mabasi yaendayo kasi hautakuhusu?
 
Mbona uko nje ya mada? Mada ni kunyanyasika kwenye mabasi ya daladala! Au wewe hunyanyasiki? Na ukombozi wa mabasi yaendayo kasi hautakuhusu?

wewe nawe ni kama chizi hayo mabasi mmeweka nchi nzima zenye foleni na au wewe ni kapuya umekuja kupima upepo kuhusu lile benz kuukuu ulilohonga?
 
Pamoja na maneno yako mazuri na yenye ukweli lakin uko nje ya mada mkuu.....mada ni kunyanyasika na mabasi ya daladala....hebu soma vizuri mada kasha utanielewa.

Nimekuelewa na ninacho maanisha mimi pamoja na kuisifu sisiem hivyo bado hawajaleta solution ya foleni ndefu katika jiji, wameleta mradi kwa ajili ya masilahi fulani.
 
Nimekuelewa na ninacho maanisha mimi pamoja na kuisifu sisiem hivyo bado hawajaleta solution ya foleni ndefu katika jiji, wameleta mradi kwa ajili ya masilahi fulani.

N vipi kuhusu manyanyaso kwenye madaladala? Au hamuyaoni kuwa ni issue kwa kuwa tu ccm inaanzisha miradi ya kuondoa manyanyaso hayo? Hiyo mada ya foleni anzisha thread uzungumzie hilo nasi tutachangia.
 
N vipi kuhusu manyanyaso kwenye madaladala? Au hamuyaoni kuwa ni issue kwa kuwa tu ccm inaanzisha miradi ya kuondoa manyanyaso hayo? Hiyo mada ya foleni anzisha thread uzungumzie hilo nasi tutachangia.

Wewe vipi? Mbona umengangana na daladala tu, je sisi tusio tumia dala dala hiyo Ccm imetusaidia vipi katika kutuondolea foleni, kuna mambo mengi serious Ccm imeshindwa kutayatatua inakimbilia kwenye project za kitoto.
Je hayo mabasi yenu ya kwenda kasi yakija ina maana daladala zote zitakuwa hazina kazi? Kisha hao makonda na madereva mnaenda kuwapa kazi gani? Hebu pisha huko, unakuwa mshabiki mpaka unakuwa kipofu
 
Wewe ni Kisena wa Simon group au Simba wa Pride wenye mradi wa UDA waliouasili na kuugeuza mabasi yaendayo kasi? So unapima upepo kama mradi utapokelewaje siyo? Tayari mmekwisha shindwa kabla hata mradi haujaanza kurun! Na hilo ndo kaburi lenu nyie manyi.nyi.emu kwa mkoa wa Dar. Na hivi unavyotetea huduma zitaboreka ni miji yote ya Tanzania? Au hiki chama kipo Dar tu eeh! Hujitambui bado!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…