Aliyekuwa Kada wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge mstaafu wa Kilwa, Selemani Bungara maarufu Bwege amesisitiza kuwa mabadiliko hayawezi kuzuiwa na mtu yeyote, amedai kuwa kitendo cha Chama cha CCM kuzuia mabadiliko kwa kutumia nguvu ya dola yanasababisha uvunjifu wa amani, ameongeza kuwa hata kitendo cha kulazimisha mabadiliko yatokee, yatasababisha uvunjifu wa amani.
Ameyasema haya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Manzese, jijini Dar es Salaam, Oktoba 18, 2025.