Bunge letu halina 'meno'

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Inapowasilishwa hoja kubwa kabisa Bungeni, Bunge hutenda kazi yake ipasavyo. Wabunge huchachamaa na kujifungua hadi kutoka minyororo ya vyama vyao.Husema kwa kukemea na kufoka na hata kutajana kwa majina. Hoja hiyo hujadiliwa kwa hisia kali na 'wapiganaji' hujitokeza. Mwisho wa yote hakuna la maana. Sanasana sakata husika huzimwa kabisa kwa kujiuzulu kwa wanaotajwa Bungeni au kwenye Ripoti husika.

Najaribu kukumbusha mifano michache. Hoja ya Sakata la Richmond tulishuhudia mengi.Kwa kusikia na kuona.Kwa kuambiwa na kuahidiwa. Bunge liliazimia-likatoa Maazimio mengi yakutosha na yenye lengo la kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika Richmond. Halafu,kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.Bunge halina tena meno ya kumalizia kutafuna mjadla wake.

Likawasilishwa sakata la Operesheni Tokomeza. Mjadala ukapamba moto na tukashuhudia mengi. Kama ilivyo ada,wakajiuzulu mawaziri watatu na hali ikawa shwari. Maazimio mangapi ya Bunge juu ya Operesheni Tokomeza yametekelezwa hadi sasa zaidi ya Kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi kulikofanywa na Rais? Bunge lakosa meno.

Juma hili likajitokeza suala la UDA. Bunge likashuhudia sarakasi za kauli kutoka wakubwa mbalimbali wa Serikali.Kuanzia Naibu Waziri wa Fedha-Adam Malima, Waziri wa OWM (Sera na Uratibu wa Bunge) William Vangimembe Lukuvi,Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Mwita Werema na Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe. Bunge, kupitia kwa Naibu Spika Job Ndugai, likaitaka Serikali ikae chini na kutatua mkanganyiko uliopo UDA. Ukimya utafuata. Bunge halina meno.

Kimsingi, Bunge ni mhimili muhimu wa kinchi. Una nafasi yake katika kuiwajibisha Serikali. Ifike mahali Maazimio au Maelekezo ya Bunge yapewe kipaumbele katika kuyatekeleza ili Bunge lionje ladha halisi ya uwepo wake. Kuyapuuza maazimio na maelekezo hayo ya Bunge ni kulinyong'onyesha Bunge na kulichora kama 'kijiwe cha stori na sanaa za jukwaani'.
 
Tena afadhali BUNGE la chama kimoja lilikuwa na uwezo wa kuiwajibisha serikali kuliko hili la leo.
 
Lina wenye meno makali sana ya kutafuna kodi za wadanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…