KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) bila kujali tofauti za vyama vya kisiasa imeisi a utendaji wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kutokana na kujipanga kimkakati katika kuboresha huduma zake, zikiwemo za kuongeza marubani kutoka 10 hadi 30 na kuongeza wahudumu kwenye ndege kutoka 84 hadi 124.
Wabunge wa kamati hiyo kwa umoja wao pia wamemsifu Rais John Magufuli kutokana na dhamira yake ya dhati ya kulifufua shirika hilo ambalo lilikuwa katika hali mbaya kwa kununua ndege ambazo sasa zinafanya kazi kusarisha abiria nchini.
Akiwasilisha ripoti ya utendaji wa shirika hilo mbele ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Emmanuel Korosso alisema shirika hilo limeweka mpango mkakati wa miaka mitano ambao unalenga kulipandisha shirika hilo. “Pia kuongeza umiliki wa soko kutoka asilimia 2.5 ya sasa hadi kukia 24 ikapo 2021/22 kwa ajili ya kuhakikisha shirika linaendelea kujipanua ndani na nje ya nchi katika kutoa huduma bora zenye ushindani,” alisema.
Alisema katika Mpango Mkakati wake wa miaka mitano 2016/17 hadi 2021/22, ATCL inakusudia kuongeza idadi ya abiria na kukia 720,000 ambao wataongezeka kutokana na kuongeza ndege nyingine na kuongeza njia ya kusarisha abiria. “Shirika linakusudia kupanua soko lake ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Kati, Kusini mwa Afrika na Magharibi mwa Afrika pamoja na kuingia katika soko la India,” alisema. Alisema shirika limejipanga kimkakati kwa kuendelea kuboresha huduma zake, ikiwa na pamoja kuongeza idadi ya marubani kutoka waliopo sasa hadi kukia 30.
“Mkakati ni kuendelea kupunguza utegemezi wa uendeshaji kutoka asilimia 94 ambayo inachangiwa na abiria, mizigo asilimia nne na barua asilimia mbili, ili kuendelea kupunguza utegemezi wa mapato na kushuka zaidi kama ilivyo katika nchi nyingine,” alisema. Mkurugenzi Mwendeshaji na Osa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, alisema shirika hilo linaendelea kununua ndege na nyingine mbili zitakuja mwishoni mwa mwaka huu, lengo ni kulipanua soko la usari wa anga ili Watanzania watumie ndege zao.
Alisema tayari imeshajipanga kwa kuongeza na kutoa mafunzo kwa wahudumu ndani ya ndege 84 waliopo na mkakati ni kuongeza wengine 40 na inataka kuwa na wahudumu jumla 124 waliobobea kimafunzo, watanashati, weledi na wenye kuitangaza sifa ya Tanzania. Alisema kutokana na kuboresha huduma zake kumekuwa na ongezeko la abiria katika kipindi cha mwaka 2018/19 kutoka 206,000 hadi 517,000 sawa na ongezeko la asilimia 150, kitendo ambacho kinalifanya shirika hilo lizidi kupanua soko lake ndani. Alisema ikapo Desemba, mwaka huu, shirika hilo ninatazamia kuongeza ndege nyingine mbili ili kuwa na ndege tano ambazo zitaongeza safari za ndani ya nchi na sasa zinafanya safari za nje ya nchi.
Alisema mkakati ni kujipanua kwanza katika soko la ndani, lakini pia tayari imeanza safari za Bujumbura (Burundi) na Entebbe (Uganda) na Comoro, pia inapanga kuanza safari za Johannesburg (Afrika Kusini), Harare (Zimbabwe), Lusaka (Zambia) na Lilongwe (Malawi) na Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuangalia soko la Afrika Magharibi kama Lagos (Nigeria) na Accra (Ghana).
Alisema katika mkakati wa miaka mitano katika soko la ndani, shirika linataka kuimarisha soko la Mwanza yaani Kanda ya Ziwa ambayo hivi sasa ina abiria wapya zaidi ya 500 sawa na asilimia 30 ya abiria wote nchini. Alisema shirika hilo ikapo 2021/22, linapanga kuwa limeongezeka vitega uchumi kwa kuwa na ndege nyingi, kupanua umiliki wa soko na na kuboresha mifumo ya mapato na kupunguza gharama na kupata faida kuwa ya kuweza kusimama kwa miguu yake. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Zainabu Vullu alipongeza jitihada zilizofanywa na uongozi wa shirika hilo ambao umeanza utendaji uliobora tangu mwaka jana.