Kuvaa raba za rojamila, maradona, ziko na DH na kaunda za mchelemchele. Wadada walikua nacraba flani nyeusi zina shingo kidogo zinaitwa Loso, basi nikiwa std 4 nikaiba za sister nikaenda kuchezea mpira. Kwa kuwa ni kijijini na almost watoto wote mnacheza peku, nilikamua sana siku hiyo tukashinda 5-2 na mi nilifunga matatu. Sasa kw kuwa raba zilikuwa laini sana na watoto wa kijiji wako sugu zilichanika vibaya mno. Kilichonikuta huko home sina hamu ya kusimulia leo aisee
Mi naona hawa watoto wa siku hizi kupata div 5 na div 4 za point 40 kuna mambo mengi yanachangia. Kwa mfano hata michezo ya watoto ya asili imepungua sana ukikompea na sisi wa enzi hizo. Mambo ya kombolela, mdako, nage, kuwinda kw manati. Kuendesha ma-ringi, baiskeli za miti, nyumba za udongo, magari ya mabati na maboksi n.k. vyote hivi vilikuwa brain activators. sasa siku hizi ni tamthiliya, bongo movie, play station n.k. eti kuna hadi tuition za chekechea. Nadhan I consider myself privillaged to be born by that time...
Ayaa nimesahau yale mashati ya bawama. Nyuma yanakuwa na rangi moja sanasana nyeusi afu mbele yanakuwa ya maua ya rangi mchanganyiko...
Wale wenye hizo title hapo juu waliozaliwa miaka ya 1978-84..walikuwa wana sifa za pekee ambazo ukiziona tu unawajua. Yaani zile za kumfanya aonekane mtu 'mjanja'. Mi nitataja baadhi kisha endelezeni.
Wanaume:
1. Kuvaa suruali za 'Tokyo, Van Basten'
2. Kubeba mabegi ya 'Montana'
3. Kutembea na 'walkman'
4. Kuchomeka t shirt au shati kwenye mkanda.
5. Kuvaa raba oversize
6. Kunyoa kwa kuchonga nywele za pembeni tuu.
7. Endeleza...
Wanawake:
1. Kuchoma nywele kwa kifuu/kigae
2. Kuvaa magauni/sketi za ngazi 3 na kuendelea.
3. Endelezeni nimezisahau ghafla nyingine.
kuvaa chupi za VIP na kuzikuta kifuani
kuvaa chupi za VIP na kuzikuta kifuani
kuvaa chupi za VIP na kuzikuta kifuani