Mi naona hawa watoto wa siku hizi kupata div 5 na div 4 za point 40 kuna mambo mengi yanachangia. Kwa mfano hata michezo ya watoto ya asili imepungua sana ukikompea na sisi wa enzi hizo. Mambo ya kombolela, mdako, nage, kuwinda kw manati. Kuendesha ma-ringi, baiskeli za miti, nyumba za udongo, magari ya mabati na maboksi n.k. vyote hivi vilikuwa brain activators. sasa siku hizi ni tamthiliya, bongo movie, play station n.k. eti kuna hadi tuition za chekechea. Nadhan I consider myself privillaged to be born by that time...