BRASIL Vs SPAIN

hivi kuna tv yoyote Bongo itaonyesha mechi hiyo na kama kuna mtu anayejua mtanange utakuwa saa ngapi?
 
Super sport 7 na 3. Saa 10 usiku kwa TZ.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Huo muda kwa kweli utatushinda wengi maana kesho yake itakuwa jumatatu. Btw naipa nafasi spain kwani wako vizuri sana na wana uzoefu wa kucheza fainali tatu kubwa mfululiza na kushinda zote
 
Ni brazili bingwa...kwa nini kadr mechi znavyoendelea brazil inaimarka ila kadri mechi znavyosonga mbele spain inashuka kiwango..brazil ilishajiandaa kisaikolojia kukutana na spain
 
Kama na WC masaa yatakuwa haya,wengi tutapoteza ajira zetu.....
Haha hahahahaa tehe tehe, kama bosi wako anapenda soka inabidi mtafute kijiwe muwe mnaangalia wote, mkiwa wote hadi night kali hawezi kukufukuza kazi.
 
Naipenda sana Brazil ila naona kama Spain watachukua ndoo
 
Nasoma maoni ya watu huku ninacheka sana. Yani Brazil hii ya sasa imfunge SPAIN? Hizo ni ndoto za mchana kwani spain wanacheza mchezo wa kasi na wa usahihi zaidi kitimu jambo ambalo brazil hawawezi na wanategemea kipaji cha mchezaji mmoja mmoja. UTABIRI WANGU SPAIN 3 BRAZIL 1
 
Hiyo mechi cyo rahsi kihivyo kaka..na kama umeangalia mech za Brazil tangu kombe limeanza utajua huo mpira hautakua mrahisi kihivyo..
 
Nadhani mechi itachezwa saa 5 usiku. Brazil walikuwa wanawashangilia sana Italy ili washinde maana wanaelewa wazi mlima wa Spain ni mkali mno kwao kuukwea, watapigwa kirahisi sana, siku hiyo yule NEEMA atageuka ASHURA na sifasifa zake, Spain wana kila sababu, nia na uwezo wa kuchukua hili kombe maana wao ni mabigwa wa kila kitu kwa uwezo wao sio bahati kuanzia WC, EURO, CONFDRTN, U - 20, U - 17 mpaka U - WEAR (Shakira).
 
Haha hahahahaa tehe tehe, kama bosi wako anapenda soka inabidi mtafute kijiwe muwe mnaangalia wote, mkiwa wote hadi night kali hawezi kukufukuza kazi.

Tabu ni kwamba mpira unaenda poa ukiwa nna maji taka ya Ilala(TBL)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…