Kuna mazungumzo yanafanyika kwamba David Haye apigane na mmoja wa hao majamaa.
Yupo yeye Klitschko halafu kuna Wladimir na Vitali. Pambano hilo linatarajiwa kufanyika mwakani pale Wembley na watu 90,000 wataleta 20 million.
Lakini kabla ya hapo itaabidi alinde mkanda wake kwa kupigana na John Ruiz hiohio mwakani inazungumziwa kwenye ukumbi wa 02 Arena uliopo mashariki mwa London.
Ila hawawezi kupigana kabla ya mwezi May kwani bado David atakuwa akiugulia mkono wake wa kushoto ambao aliumia kwenye mpambano wa jana.
Wladimir, anashikilia mikanda miwili ya IBF na WBO ambayo ni sawa na ubingwa wa uzito wa juu.
Vitali, ana ubingwa wa WBO na ndie anaehofiwa kwa sasa na amesema yupo tayari kukabiliana na David Haye.