BONGO, HATA SHERIA YA KUTUOKOA TUNATAKA KUIGOMEA!

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,092
Reaction score
865


Serikali imeanzisha mfumo wa point kwa madereva wanaovunja sheria za barabarani. Lengo ni rahisi: ukifanya makosa, unapunguziwa point; ukizidisha makosa, leseni yako iwe hatarini.

Lakini hii ni Bongo.

Badala ya kusema “tufuate sheria,” tayari tunasikia: “Tutagoma!”

Yaani tunataka barabara salama, lakini tusiguswe tunapovunja sheria. Tunataka foleni zipungue, lakini tuendelee kukatiza njia. Tunataka ajali zipungue, lakini dereva anayefanya makosa mara kwa mara asipoteze leseni. Tunataka nidhamu lakini kwa hiari!

Halafu anakuja mwanasiasa: “Madereva wanaonewa!”
Anakuja mwanaharakati: “Msikubali!”

Lakini nani anatetea abiria anayekufa kwa uzembe? Nani anatetea familia inayopoteza mzazi kwa dereva asiye na nidhamu? Nani anatetea maelfu ya watu wanaopoteza saa zao kwenye foleni kwa sababu kila mtu anataka kuendesha anavyotaka?

Kuna mentality ambazo hazibadilishwi kwa semina, mabango na “tafadhali.” Zinahitaji sheria yenye meno.

Kigali haikupata nidhamu kwa miujiza.

Singapore haikujengwa kwa kuwaambia watu, “ukijisikia, tafadhali fuata sheria.”

Nidhamu ya umma hujengwa kwa sheria zilizo wazi na enforcement isiyochagua mtu.

Tanzania haihitaji dictator wa kisiasa. Inahitaji dictatorship of the law.

Sheria iwe dictator kwa dereva, bodaboda, daladala, mwanasiasa, mwanaharakati, tajiri, maskini na hata polisi mwenyewe.

Point system iwe transparent, iwe na haki ya kukata rufaa, ushahidi wa makosa utumie teknolojia, na isiwe mradi mwingine wa rushwa. Lakini baada ya kuweka safeguards hizo, vunja sheria, poteza point. Rudia, poteza leseni.

Simple.

Maana Bongo tumefika mahali pa ajabu:

Hata sheria inayotaka kutuokoa na sisi wenyewe tunataka kuigomea!
 
Mbona Katiba ya JMT ambayo ndo sheria mama haifuatwi na serikali? Wewe vipi?
 
Ndugu mjumbe,,,,,Madereva na gari za serikali watungiwe sheria za kuwabana waache kutanua na kupita kwenye mwendokasi.
 
Ni muda Sasa umepita tangu nikutane na mada yenye akili kama hii. Huyu akijiita great thinker simbishii.....Kuna watu humu Wanashusha mada Kila siku lakini ni zote ni ujingaujinga tu kuhamasishana kupiga kelele mahakamani au wa kumtukana Samia.

Naunga mkono mleta mada, tunahitaji serikali ngangari inayosimamia Sheria na taratibu bila kuyumba na wananchi wasioendeshwa kimihemko ya wanaharakati uchwara.
 
Point zinakatwa lakin hakuna kuongezeka je dereva akifikisha gar na abiria salama anaongezewa point ngap,

Kila baada ya 15-20km kina traffic alafu unakuta barabara ina tuta kubwa kama la viazi, na kabla ujakuta hilo tuta Kuna vi Rasta vikali kinoma na ndio chanzo cha kuaribu magari(shockuo, spring, bush na rim) Bado Kuna mstar wa zebra nyuma Kuna kibao cha 50 alafu unakuta traffic kajificha na tochi yake huu sio ujunga wandugu
 
Wanaofaidika unahisi ni nani kama sio matraffic wenyewe, tayari wana nguvu, sahv ndo watatengeneza maghorofa kabisa
 
Tatizo ni wasimamia sheria kukutebgenezea makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…