ndugu zangu pale suala la bodi ya mikopo ya elimu ya juu lina ukakasi mwingi sana...Mimi mwaka 2014 nilienda wakanipa print out kwamba nadaiwa 23M,nimelipa weeeee kwa miaka 6 mpaka mwaka huu mwanzoni deni halipungui....nikaenda tena pale bodi ya mikopo nikapewa statement nyingine deni sasa limefikia 72M..... nimepambana nao kujua nini kimetoa lakini mpaka ukienda kwa huyu anakuelekeza kwenda chumba kingine floor nyingine na mpaka sasa wanapiga tu danadana.
kwa ufupi kama mna ndugu wanaotegemea kwenda university chonde chonde washauri sana sana kopa mtavyoweza kawasomeshe watoto private...bodi ya mikopo ya Tanzania imejaa ubabaishaji