Salaam kwa wana JF wote!
Nimekuwa na Samsung Digital Camera (ES70/Es71) kwa miaka miwili sasa. Juzi kuna my friend aliiazima ili akaitumie,nilimpa kwa nia nzuri tu. Cha ajabu ile kunirudishia nimeikuta Screen ya Camera ina madoa ya mviringo matatu meusi (black/dark spots) na nimemwuliza kulikoni?? Jamaa ananiambia naye anashangaa kusikia tarifa kama hiyo....in short ameniruka kabisa,si unajua wabongo??
Dokezo: Picha zinatoka vizuri tu!
Maswali yangu: Madoa haya yanatokana na nini? Je nitayaondoaje?
Yaani display ya hii camera imekuwa haipendezi sababu madoa haya ndo yanayotawala almost 1third ya the whole screen!
Nawasilisha.