una represent serveu zeroAbsolutely?
Siyo kuishia kutukana tu, bali unaweza hata ukapata kichaa kutokana na msongo wa mawazo.
"Ukiwa na akili timamu kabisa, kuishi Afrika ni kazi kubwa na ni mateso makubwa sana."
Mnyika anajifanyaga Mdadisi na Mtafiti 😂
huna akili hyu botha utamujua ajeNiliwambia watu hili wakasema mimi si mzalendo.
PW Bother 1985
Non senseKiongozi akiwa nje kikazi kuna kitengo cha habari kwa kiongozi husika kuonyesha anafanya nini huko aliko,.
Mfano Rais Samia alipo mkutano wa mazingira na tabia nchi wa kimataifa kuna picha tunaziona na anachozungumza tunakisikia na kukisoma,kulikoni kwa Makamu wa Rais Dr Mpango?
Zinduka, mleta uzi yuko sahihi, serikali inaficha jambo,
Swali linabaki kwako, kuna faida kuficha?,maana serikali watumishi wake huapa kutunza siri za serikali,pengine na la ugonjwa pia ni sirikali
You may be a PhD holder but still an IGNORANT.Mbona wana ma PhD,masters na madigriii?
DeplrorablèYou may be a PhD holder but still an IGNORANT.
Remember: Education is the level of knowledge and skills that remains in your mind after forgetting all other things that you have studied.
Kwamba Makamu wa Rais alienda nje kikazi bila kujilikana alienda kufanya kazi gani na nchi gani? Au alienda kwenye kazi zake binafsi siyo ya Umma?Embu acha porojo zako hapa zisizo na mshiko .kwanza andiko lako umelikoroga sana na kulichanganya na kujichanganya sana ambapo sijuwi hata kama wewe mwenyewe unafahamu ulichoandika .
Unaposema kuwa watoa taarifa ni waongo halafu ukashindwa kuweka ukweli wenye ushahidi unataka tukuelewe vipi? Unataka tuelewe nini? Wewe mwenye kuujuwa ukweli kwanini usiuweke hapa kuthibitisha huo uongo unaousema? Hoja hupingwa kwa hoja. weka hoja yako ya ukweli ndio watu wajuwe kuwa taarifa walizopewa ni za uongo.
Lakini kama huna huo ukweli unaousema ambao ni tofauti na taarifa iliyotolewa basi nakutaka ufunge mdomo wako na kutulia tu kuliko kuendelea kuropoka ropoka hapa.
Tukiambiwa tatizo la nchi zetu kutoendelea ni ukosefu wa utawala bora na siyo bora utawala (good governance), tunakimbilia kusema hayo ni matamshi ya kibeberu! Hawa viongozi wetu wanasahau kuwa ni viongozi wa wananchi na wanawajibika kwa wananchi. Tumwombe Mwenyezi Mungu Atukumbuke kwenye hili suala la utawala bora!Kuna mambo huwa yanafanywa na baadhi ya viongozi wetu, mpaka unajiuliza tunaongozwa na watu wa namna gani! Maana ni kama hata kwenye kile kiwango cha akili ya kawaida, hawamo.
Nchi zetu hizi hazipati maendeleo kutokana na kukosa viongozi katika maana ya viongozi. Kuwa kiongozi maana yake ni wewe kuwaonesha njia unaowaongoza. Kama kiongozi unakuwa mwongo maana yake utatengeneza watu wengi waongo. Kiongozi ukiwa mwizi, utatengeneza wevi wengi sana. Lakini pia kiongozi ukiwa mwadilifu utatengeneza waadilifu wengi. Kiongozi ukiwa mkweli, utatengeneza watu wakweli wengi.
Jamii yetu kujawa na watu wengi wa ajabu ajabu, kuwa na watendaji wengi Serikalini wevi, wafujaji, waongo, kunaashiria ndivyo walivyo wakuu wao.
Ninachojiuliza, hivi hawa watawala wetu kwa kuyapata madaraka huwa wanaamini wameuaga ubinadamu, wao sasa siyo wanadamu? Na kwa vile wao ni juu ya wanadamu, hawawezi kuugua wala kufa? Nadhani kwa kuamini kuwa wao ni zaidi ya wanadamu, ndiyo maana wengine huwa wanaiba mpaka wanakufuru. Mtu anaiba kiasi hata akiishi miaka 2,000 hawezi kumaliza utajiri wa wizi alioutengeneza.
Mimi naamini, kwa mwanadamu kuumwa au hata kufa, ni mambo ambayo humpata mwanadamu yeyote, na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia. Kuumwa au kifo siyo aibu na wala siyo kosa la mgonjwa au marehemu. Kama haya ninayoyasema ndiyo ukweli, kwa nini watawala wa Tanzania, kiongozi akiugua huwa wanapenda kusema uwongo?
Hayati Magufuli wakati anaugua, katikati ya minong'ono kuwa Magufuli ni mgonjwa, watawala waliamua kusema uwongo kuwa Magufuli yu mzima. Akiwa tayari ameaga Dunia, baadhi ya viongozi waliendelea kusisitiza kuwa yumzima.
Angalao Kikwete yeye aliamua kuweka wazi alipokuwa anaumwa, tena akaenda ndani zaidi hadi kuelezea alikuwa anaumwa nini.
Kule South Afrika, Mandela alipougua mafua makali, nchi ilitangaziwa. Baadaye alipougua tena na kulazwa, wananchi walipewa taarifa, na baadaye kupewa taarifa ya maendeleo yake karibia kila siku. Mseveni alipougua, wananchi walitangaziwa. Malkia Elizabeth alipovunjika mfupa, wananchi walijulishwa.
Hawa wa kwetu kusema uwongo kiongozi akiugua wanataka kutuambia kiongozi siyo mwanadamu, na hivyo haguswi na maradhi, ajali wala kifo?
Kuna minong'ono kuwa Makamu wa Rais ni mgonjwa, na kwamba yupo nje kwa matibabu, lakini watawala wanawadanganya wananchi kuwa yupo nje kikazi.
Kama ni kweli kuwa Makamu wa Rais anaumwa na yupo nje kwa matibabu, hawa wanaosema yupo nje kwa ziara ya kikazi, kweli wana akili timamu? Na kama hawana akili timamu, nchi inayoongozwa na watu wasio timilifu, mwisho wake ni nini?
Hilo nalo Mwanangu Ummy na timu Yako mwende mkalitizame!Kuna mambo huwa yanafanywa na baadhi ya viongozi wetu, mpaka unajiuliza tunaongozwa na watu wa namna gani! Maana ni kama hata kwenye kile kiwango cha akili ya kawaida, hawamo.

Lazima tujulishwe,yule ni Makamu wa Rais wa nchi siyo Makamu wa Rais wa bao kule Uswazi!Kazi kweli kweli
Kuna sheria inayosema ni lazima kujulishwa walipo Viongozi wetu wakati wote?!