Location yenye shughuli nyingi za kiofisi, chuo au shule, karibu na ofisi za serikali au vituo vya polisi nk.
Vifaa bora na huduma bora, hapa kwenye huduma bora zingatia kua watu wengi hawaelewi vizuri mambo ya stationary hivyo kua na lugha nzuri, uelewa wa haraka wa mteja anataka nini kwa wakati huo uwe mwepesi wa kuelekeza au kuuliza pale unapoona anachotaka mteja sio kitu bora au sahihi.
Kama ni sehemu changamfu sio mbaya ukaweka na kafriji uuze vinywaji pia, kama ni karibu na shule/ofisi za serikali basi nashauri weka na vinywaji na bites ili uokote zile chenji za mia au miambili za wale wasiopenda kubeba chelechele, hii pia itakusaidia kutokua na uhaba wa chenji.
Nawasilisha kiongozi.