Habari yako mkuu.
Biashara ya nazi ina faida yake endapo utapata mtu mwaminifu wa kukusaidia kununua nazi zilizokomaa vizuri . Ukipata nazi nzuri unaweza nunua 650 au 700 ukauza 1200-1400 kwa bei ya jumla.
Vile vile ina hasara zake maana ukiwa huna uzoefu na nazi, unauziwa nazi zilizovundikwa ambazo hazijakomaa ukizivunja unakuta ndani ni madafu matupu hapo unakuwa umepigwa na wengi wanapigwags hivyo. Pia hakikishs hazilowi wala kugusana na maji hata kidogo na uhakikiahe zina pata hewa vizuri kwenye magunia laasivyo zinaozs ndani unakula hasara.
Nasisitiza nenda kununua na mtu mzoefu na mwaminifu anayeweza kutambua nazi iliyokomaa na ambayo imevundikwa tu bila kukomaa.