Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

ngora

Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
76
Reaction score
136
Habari wanajamii wenzangu,

Ningependa kupata mawazo hasa kutoka kwa wajasiriamali. Mimi nimekuwa mchimbaji mdogo katika eneo moja hapa nchini kwa miaka 9. Kwa bahati, wiki iliyopita nilipata dhahabu iliyonipatia zaidi ya milioni 200.

Kwa kuwa kazi ya uchimbaji ni ngumu, nimefikiria kuachana nayo na kuanza biashara. Naomba ushauri, kwa mtaji wa zaidi ya milioni 200, ni biashara gani naweza kuanza ambayo ina nafasi nzuri ya kunipa faida?
 
Kwasababu unayajua madini vizuri kwanini usiwe dealer? Unanunua kwa wachimbaji wadogo halafu unawauzia wengine.
 
ni ngumu hii biashara na kuwa dealer mtaji mdgo na kutapeliwa rahisi sana
 
Tafuta biashara yoyote uanze na mtaji mdogo kama 20m halafu kuwa nayo mpaka ufikie mtaji wa 200m. I did the same,ila kuanza na 200m kwa kitu kipya, sijui.
asante kwa wazo
 
Nikopee milioni 10 tu mkataba wa mwaka nakurudishia milioni 15.

Nikuonyeshe cha kufanya nina wazo lakini halina mtaji.
 
Biashara isiyokuwa na risk au yenye risk kidogo ni kununua kiwanja na kujenga nyumba yenye thamani ya milioni themanini afu jaribu kuiuza kwa milioni mia moja na kumi au pangisha.Kama unamiliki nyumba na mahali pa kuishi na hauna majukumu makubwa kula bata tu maisha yenyewe mafupi hizo biashara waachie wahindi na waraabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…