Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 83
Una mtaji -fedha kiasi gani kwa kuanzisha hill wazo lako
Wazo zuri na yote yanawezekana ni kujipanga tu
Wazo zuri mdau, pigana asibuhi
mimi ntakusupply mashudu kama wataka kuanzi tani 25
Wakuu habari zenu,
Kwa muda nimekuwa na hamu ya kuanzisha biashara ya Chakula cha mifugo, kwa ajili ya wafugaji. Lakini mbali na chakula nitauza vifaa vya ufugaji na nitakuwa wakala wa vifaranga vya kuku wa kisasa, kienyeji na kwale na nitakuwa natoa huduma ya utotoleshaji vifaranga.
Chakula nitakachouza ni pamoja na mahindi, dengu, mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba etc, na vile vile nitakuwa wakala wa kuuza chakula cha kuku wa kisasa laani layers na broilers. Hii ni plan yangu ya muda mfupi lakini baada ya muda wa mwaka mmoja nataka nianze kupack chakula changu mwenyewe, nadhani by then nitakuwa nimeshanunua mashine ya kutayarishia vyakula vya mifugo na vifaa vya packaging.
Naomba mwana JF mwenye uzoefu na biashara hii anipe ushauri wa nini cha kufanya, wapi naweza kupata bidhaa hizi kwa bei nzuri itakayo niletea faida nzuri. Na changamoto zake kwa ujumla.
Location ninayo na ni nje ya mji, kwa hiyo kwa ufupi kodi ya pango ninayo, budget ya promotion ninayo, Bei ya kununua bidhaa ninayo na Bei za kuuzia ninazo tayari.
Naombeni ushauri wenu.
Wasalaam Mambo Jambo, Dar es Salaam
Mkuu Elungata heshima mbele, uko mkoa gani, bei zako zikoje mkuu na vipi unagharamia usafiri mpaka store kwangu
Wazo zuri anza kwa kufungua kampuni au jisajili kibiashara kwani kuna fund ziko nje nje kwa miradi kama yako kikubwa uwe umeanza....
Wazo mujarabu
Mkuu Elungata heshima mbele, uko mkoa gani, bei zako zikoje mkuu na vipi unagharamia usafiri mpaka store kwangu
Biashara ya Chakula cha Mifugo inalipa hata zaidi ya ufugaji wenyewe..., Margins za kutosha..
Ila wachanganyaji / watengenezaji wengi wa Bongo wababaishaji tu..., inabidi feed value iwe inapimwa kabisa maabara (protein, Fiber, Carbohydrates n.k.) sio tu kutumia known feed value ya kitu fulani..
Kenya kuna maabara kabisa wanapima na wanahakikisha uchanganyaji na utengenezaji ni wa makini na hakuna contamination, sio unamuuzia mteja anakwenda kuua mifugo yake.....
Tanzania zipo maabara za kupima hivyo vyakula vya mifugoNi kweli kabisa, hivi ni vitu vinavyotakiwa kufanyiwa kazi ili wafugaji wafuge kwa tija na iwe kweli Ufugaji wa Kibiashara, asante kwa mchango wako