BENKI KUYUMBA NCHINI!

Sio Benki tu zinayumba hata Ndoa nyingi zinayumba hadi zinazama.
Uchumi unakuwa kwa kasi, wanaoyumba wanashindwa kwenda na kasi ya uchumi.
 
Kwanza kabisa inabidi tuangalie ni kitengo gani katika benki zimeteteleka.

Mpaka muda huu taarifa zilizopo zinaeleza mikopo mingi imeshindwa kulipika ndani ya wakati. Hivyo masuala ya huduma kwa wateja sitojadili.

Hii imepelekea BoT kwa maagizo ya mkuu kushusha riba za mikopo, mathalani tatizo hili limeendelea inaionyesha dhahiri kuna kitu wamekosea au kuounguka kwenye dawa ya tatizo.

Maoni binafsi: (yasio weza tekelezeka maana kuna watu wanaamini wanajua kuliko wenzao hata kabla ya kuwasikiliza)


1. Kiwango cha riba kilinganishwe na ukuaji wa uchumi kwa muda muafaka uliopo. Ikiwa uchumi unakua kwa 7% basi mikopo iwe 7% pia katika riba. Kama ni ngumu kumeza kila sekta iwe na riba yake kulingana na kasi ya ukuaji.

2. Benki Kuu ishauri na kushinikiza mikopo itolewe kwenye sekta zinazofanya vizuri tu. Sekta zilizo dolola ni mashimo ya kupoteza fedha za mikopo, hivyo mabenki wapunguze kiasi na mikopo inayo tolewa huko.

3. Mifumo na utaratibu wa tozo mbali mbali ziangaliwe upya ili zinaendane na maelengo ya maendeleo. Kama tuna mpango wa kukukuza uchumi kwa 7-10%, tozo zilizopo zishuke. Mfano; makadilio na mtizamo wangu wa mwaka jana uchumi ulikua kati ya 1-3% hivyo TRA iangalie namna ya kushusha kodi za umiliki na uendeshaji wa Biashara ikitoa tija ya unafuu kwa makampuni yalio ajiri watu wengi katika mafungu. Mfano biashara ikiwa na watumishi 5 tozo yake iwe juu kuliko biashara yenye watumishi 10 ili kuhamasisha watu waajiriwe zaidi katika biashara. TRA haina haja ya kudai tozo zaidi kwa makampuni yalio ajiri watu wengi maana fedha hizo zinaweza wafikia watu kwa njia ya mishahara.

Jioni njema wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…