BASATA Awamu ya Tano imewaacha

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,563
Reaction score
91,855
BASATA HAIENDANI NA KASI YA AWAMU YA TANO.

Na, Robert Heriel.

Baraza la Sanaa la Taifa - BASATA, ni moja ya Mabaraza hapa nchini ambayo hayalisaidii taifa kama inavyotakiwa. Ni baraza ambalo kwa muono wangu viongozi wake wapo kwa mazoea pasipo ubunifu wowote kwa manufaa ya taifa.
Viongozi wake sio watu wa kujiongeza iwe kwa kuishauri serikali namna bora ya kuinua sanaa ya Tanzania na kulisaidia taifa hili.

BASATA inapaswa iangaliwe na kufanyiwa marekebisho ili iwe na tija kwa taifa hili. Viongozi wake wachekiwe ikiwezekana watolewe na kuwekwa wengine ambao ni wabunifu watakaolisaidia taifa hili.

BASATA haiendani na kasi ya Magufuli. Haiendani na awamu hii kabisa. Yaani safu ya uongozi Inapaswa iangaliwe upya kabisa.

Hivi BASATA inatambulishwa na nini hasa kwa Wananchi zaidi ya kufungia Nyimbo za Wasanii ambao wamekiuka kile kiitwacho maadili. Kipi kingine kinachoitambulisha BASATA kwa raia wa kawaida kama sio jambo hilo tuu?

Hata hao wasanii wengi wao wakiulizwa kuwa wanajua kuwa kuna BASATA basi watakujibu hawajui. Na wanaojua kuwa Kuna BASATA basi ukiwaambia kazi ya baraza hilo watakujibu ni kufungia nyimbo zisizo na maadili. Nina uhakika zaidi ya 80% ya wasanii hawaijui BASATA. Na kama wanaijua hawajui kuwa hilo ndio BARAZA linalowasimamia na kuwaunganisha na Serikali.

Kitendo cha Wasanii kutokujua Majukumu ya BASATA kunatoa tafsiri kuwa chombo hiko hakitimizi majukumu yake. Kitendo cha baadhi ya wanasanaa kutokujua kuwa kuna chombo kinachosimamia kazi zao hiyo pia ni kushindwa kwa BASATA.

Kwa wasiojua tuu Kwa nchi ya Tanzania Watu wengi wamejiajiri kupitia Sanaa. Hii humaanisha kuwa Sanaa ndio kazi zao. Sanaa ni sehemu inayotegemewa kwa uchumi wa taifa hili. Sanaa ndio sekta ambayo kila familia kuna mwanakaya mmoja anajishughulisha na kazi za sanaa. Hii ni tofauti na fani zingine ambazo unaweza kuta ukoo mzima hakuna mtu mwenye fulani lakini kwa habari ya Sanaa, hakuna familia isiyotegemea sanaa.

Sanaa inatanzu zifuatazo:
> Fasihi
> Ushonaji
> Muziki
> Uchongaji
> Ufinyanzi
> Ususi
> Utarizi
> Maonyesho
> Urembo
> Uchoraji
> Ukinyozi n.k

Kila familia lazima mmoja wa wanafamilia awe na kazi moja kati ya hizo ambazo ni sanaa. Dada zetu wanapendeza kwa sababu wapo wasusi wa wanaosuka huku kwenye saluni. Bila wasusi wanawake wangekuwa kwenye hali mbaya mno. Wapo vinyozi wanaotunyoa nywele kwa mitindo mbali mbali. Wapo wanafasihi kama mimi, waandishi wa vitabu, washairi. Haya wapo wazee wa urembo wa Make up kwa dada zetu. Wapo Wachoraji tukipita kwenye mabara bara tunaona picha za kupendeza, hata mabasi ya abiria mengi yamechorwa na wao. Wote hao ni wasanii lakini nina uhakika hawajui kuwa kuna baraza linalowasimamia na kukuza sanaa zao.

Baraza limejikita na wasanii wa Muziki tuu utadhani hakuna sanaa zingine. Huku ni kushindwa kwani Sanaa ni kubwa na inavipengele vingi. Kuchukua muziki na bongo muvi wakati kuna zaidi ya sanaa zaidi ya nane zingine ni kuonyesha kuwa baraza halipo sirius na kuwasaidia watanzania.

Kutokana na ukosefu wa ajira na ongezeko la kundi la vijana wasio na ajira ilhali BASATA ipo ni ukosefu wa ubunifu. BASATA inaouwezo wa kuandaa programu za kusajili wanasanaa wa tanzu zingine kwa ajili ya kukuza sanaa hizo. Kuwasimamia na kuhakikisha wanapata elimu kuhusu sanaa zao. Na sio kudeal na Wasanii wa Muziki na Bongo Muvi Peke yao.

BASATA mjipime kwa kweli. Hamuendani na kasi ya Magufuli kabisa.

Mmeshindwa kufanya walau mambo yafuatayo:

a) Kuanzisha siku ya maonyesho ya Sanaa kila mwaka.
Mbona wakulima wanasiku yao ambayo wanaiita nane nane. Wafanyakazi, mei mosi, Wafanyabiashara, saba saba. Wakristo, chrismass, Waislam, Idd Mubarak sijui el fitri. Hizo siku zote zipo kibiashara na zimewekwa kwa lengo la biashara na kuinua makundi husika.
Tafuteni tarehe na mwezi wa kuazimisha siku ya Sanaa Tanzania kila mwaka. Hapo yatakuwepo maonyesho ya sanaa zote, sijui wasusi, wachoraji, wachongaji, wanafasihi, wanamuziki, miongoni mwa wengine.
Hapo kila kanda wataadhimisha kwenye mahali maalumu huenda ni kiwanja au ukumbi. Vijana wote wenye sanaa wataonyesha sanaa zao. Na watu watakuja kulipia kama ilivyo kwa siku za saba saba au nane nane.

b) Kuandaa Mtaala maalumu wa sanaa.
Hapa serikali nayo inabidi iangalie kwa kweli. Sanaa ni moja ya mambo yanayogusa jamii kwa haraka sana. Sanaa ni kama elimu tuu. Ni lazima iwe na Silabasi ndio mtaala utakaowaongoza wasanii katika kazi zao.
Mtaala uendane na sera ya nchi na maadili ya nchi husika.
Wasanii wanapaswa watoe sanaa zao kulingana na muongozo maalumu unaolandana na sera ya nchi. Kwa mfano sera ya nchi labda ni Tanzania ya viwanda. Ingepaswa mtaala wa sanaa utoe muongozo kwa wasanii wote kazi zao kwa sehemu kubwa zijikite kwenye masuala ya Tanzania ya Viwanda. Wanamuziki nyimbo zao nyingi zilipaswa zihusu masuala ya viwanda atleast 75% ndio zihusu mambo mengine.
Halikadhalika na waigizaji, wachoraji, wachongaji na sanaa nyingine hasa za maonyesho na zile sanaa za ghibu.
Lakini kwa vile hakuna muongozo basi utashangaa wasanii wetu wanajiingiza kwenye mitaala ya mataifa mengine. Wanajikita zaidi wakiimba mambo yanayotoka nchi za watu zaidi kuliko sera za nchi.

c) Kuwekea Vikwazo Sanaa za nje na kuzipa promo Sanaa za ndani.
Baraza linapaswa sheria zake ziweke ushuru mkubwa kwa yeyote atakayetumia sanaa ya nje nchi kuliko yule anayetumia sanaa ya ndani ya nchi. Ushuru wa mtu anayetumia sanaa ya nje uwe mara mbili ukilinganisha na yule anayetumia sanaa za ndani.
Lengo ni kutetea soko la vijana wetu waliojikita katika sanaa. Nafahamu kuwa Wanaoiga sanaa za nje ndio watakaodondosha sanaa ya ndani. Mfano wasanii wa Muziki wanaiga uimbaji wa nje mathalani wanaimba kama wanaijeria hii hupekelea wasanii wetu wengi kushindwa kutoboa anga la kimataifa. Watakaofanikiwa ni wachache wasiozidi watatu. Wasanii wetu hawawezi kujidanganya kuwa watawapita waimbaji wa Kinaijeria kwa kuwaibia. Huwezi ku-copy alafu ukamshinda uliyemuibia.
Sanaa za mitindo ya nguo, urembo, vinyozi na ususi.

Lazima watanzania wajifunze kuiga watu wa kwao na wala sio kuiga wageni. Nitafurahi kama watu wataanza kuiga unyoaji wa Samatta(kama atakuwa na mtindo), akina Diamond, Ali Kiba, n.k Nategemea kwa wenye akili hasa maeneo ya Saloon nione zaidi picha za wasanii wetu, viongozi wetu, na watu wengine wa nchi yetu. Kuweka picha za wasanii wengine kama kina Chris Brown, Lily Wyne, Beyonce n.k ni kutokuwa mzalendo.

d) Usajili maalumu upitishwe kwa wanasanaa.
Baraza lisajili wasanii wote kwa makundi yao. Wachongaji, wachoraji, washonaji, wasusi n.k. Walipie ada ya uanachama na kutambulika. Ada iwe bei nafuu
Baada ya kusajiliwa baraza liandae mpango maalumu wa kutoa bei elekezi kulingana na ujuzi na elimu ya mwanasanaa. Kwa mfano Fundi nguo yawepo madaraja matatu kulingana na ujuzi na elimu ya fundi. Daraja la kwanza bei yake iwe kati ya 10,000/= - 25,000/=, daraja la pili bei iwe kati ya 26,000/= - 50,000/=, daraja la tatu bei yake iwe 50,000+
Inamaana baraza litatoa leseni maalumu kwa fundi, kulingana na ujuzi wa fundi. Hivyo fundi atalipwa na mteja kulingana na ujuzi wake. Halikadhalika na vinyozi, wasusi n.k

e) Kila mwisho wa wiki pawepo tamasha maalumu la sanaa,
Kila kata ifikapo mwisho wa wiki liwepo tamasha litakalosimamiwa na serikali za mitaa lakini linaweza kuendeshwa na wafanyabiashara ikiwa wao ndio watakuwa wadhamin. Hapa vijana wanasanaa iwe ni wanamitindo wa mavazi, iwe ni vinyozi, wachoraji, waimbaji au wanasanaa wowote wataandaa sanaa zao na wananchi watalipia viingilio kwa bei nafuu. Hapo wengi watajipatia ajira. Wafanyabiashara mitaa hiyo watapata, vijana watakaolinda watapata ajira, wanasanaa watafaidika, bodaboda watakaoleta na kurudisha watu, n.k

F) Propaganda.
Wanasanaa wakubwa waandaliwe kwa kazi za kipropaganda hasa kuwatisha na kuteka soko la nchi za nje. Majirani. Lazima kuwe na mahusiano ya karibu baina ya wanasanaa kwa ajili ya kuliinua taifa hili. Kwa mfano msanii mkubwa wa Muziki sharti awatumie wanamitindo ya nguo wa ndani, wanasanaa wa make up, vinyozi au wasusi wa nchi zetu.
Vyombo vya habari vihakikishe nyimbo yoyote inayoponda utamaduni wa kitanzania haupandi hewani na msanii huyo achukuliwe hatua kali kwa kulichafua taifa.

Kwa mfano, kuna dogo mmoja aliimba wimbo sijui "Bongo bahati mbaya, karibu ulaya" wimbo wa namna ule haukupaswa upande kwenye chombo cha habari chochote cha watu wenye akili. Lakini kwa vile wengi wa watu ni wapumbavu ndio maana nyimbo za hivyo huachwa. BASATA nyimbo kama hizo hupaswa kufungiwa na kijana kama huyo hupaswa kukamatwa na kukaa ndani mwezi mmoja kwa sababu kaeneza propaganda kuwa bongo yaani hapa nchini kwetu sio kitu, ni sehemu ya bahat mbaya na kupasifia ulaya ambao sio kwao.

BASATA Hamuendani na kasi ya Magufuli. Ninawasihi mjitathmin. Kama hamuwezi ni bora muondoke waingie watu wabunifu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
0711345431
 
Aisee, usiku huu nyuzi ndefu hazipandi kabisa, ngoja niweke siti ntarudi kucomment kesho nikiamka.

Unforgetable
 
Kwa jinsi ulivyosema kuhusu vyeti na ada za usajili wa "wasanii" bora ungesema basata iwe kitengo cha veta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…