Barua ya wazi kwa RC Paul Makonda

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
814
Reaction score
1,490
Mheshimiwa Makonda, Salaam.

Nataka nikupe pongezi zangu za dhati kwa kasi ya utendaji wako na jinsi unavyo lipigania taifa la Tanzania. Kuna watu wanafikiria tofauti na unavyo fikiria wewe. Wewe unamawazo chanya una kipawa cha uongozi usiyumbishwe na wale wanao kukatisha tamaa. Hao wanachukia wanapoona nyota yako iking'aa kinyume na matarajio yao, hivyo wanakutafutia visababu ili kuweza kukuangusha. Wanawatuma watu waongee wanayo yaongea, amini kwamba hao ni vipaza sauti tu kuna watu walio watuma.

Wakati ukitetea hali za wamama wanao nyanyaswa Arusha sikuwaona UWT wala TAMWA wakikupongeza, umesaidia wamama wengi kupata haki zao, wengi walio najisiwa watoto wao umewapa haki hakuna aliye kupongeza! Lakini ulipomkemea yule mtendaji wa serikali kwa uzembe wa kutotekeleza majukumu yake na kufikia hatua ya kuathiri maelfu ya wananchi waliibuka na kusema kwamba umekosea na kutaka kwamba eti uwajibishwe!

Kuna watendaji waliozoea kula rushwa. Ulipoanzisha uchunguzi kwenye mifumo ya malipo ya serikali wengi hawakupenda, ni wale wanao nufaika na mfumo huu maana wanajua sasa wameumbuka kwa kuchepusha pesa za serikali, na kupitia wewe mifumo yote Tanzania nzima ni lazima ichunguzwe.

Utashangaa pale utakapo fanya vizuri hawata kupongeza, watakaa kimya ila pale utakapo teleza utawasikia kwenye vyombo vya habari wakikuchongea kwa viongozi wajuu kwa maneno ya hapa na pale.

Mkuu nikwambie kitu kimoja songa mbele usirudi nyuma wala kukata tamaa, kuna mamilioni ya watanzania wanakutazama, wanakukubali na wanaona kasi ya utendaji wako wa kazi. Wewe ni dhahabu ili uweze kung'aa ni lazima upite kwenye moto.

Nakutakia utendaji mwema katika kazi yako.
 
Makini sana
 
Sema Daudi Albert Bashite ana wajinga wengi sana wanao muunga mkono. Na mmojawapo bila shaka ni wewe mtoa mada.
Sio kweli kwamba wanaomshabikia Makonda kwamba wote ni wajinga, bali ni watu waliokandamizwa na mfumo wa uongozi wa CCM.

Anachokifanya Makonda(na hili analijua wazi) ni kwenda kinyume na mfumo uliozoeleka wa hicho chama ambao hauna tija na ambao pia wananchi wameshauchoka. Mfumo wa maneno mengi matendo kidogo, mfumo ulijaa rushwa na ulaghai pamoja na ukandamizaji.

Anapotokea mtu anayeenda tofauti ni lazima wamshabikie.

Anachofanya Makonda ni kucheza na 'mwanya'.
 
 

Haa mkuu wa mkoa wa Mayara amelala usingizi
 

Hapa mkuu wa mkoa wa Manyara amelala usingizi
 
Mnajibaraguza bure ila jueni barua ya kumfukuza kazi tayari ishaandaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…