Inawezekana jamaa aliongea kwa nia njema tu, ila inatengenezewa mazingira ieleweke kivingine.
Diamond anapigwa vita kinoma adondoke, tusichojua wabongo ni kuwa mshkaji akidondoka tunadondoka pia sisi. Chalii ametuweka kwenye ramani ya muziki ambayo hatukuifikiria kwa miaka ya karibuni kwa juhudi zake, ila sisi badala ya kum-support ndio kwanza tunampiga mawe hatari. Kuna nchi kibao hapa Africa kitu kizuri pekee wanachojua kutoka bongo ni Diamond na ushiriki wetu Big brother.
Binafsi dogo siuelewi muziki wala pozi zake, ila kila nikiskia kapiga hatua flani nafarijika kama Mtanzania na namuheshimu.
Ila sio issue, tumshushe tu halafu tuanze upya kuwapandisha tunaowapenda, tukishindwa tuanze kulaumu jinsi Nigeria walivyo-dominate game, si ndio zetu.