Barabara za mkoani

Aisee nchi hii ndio maana Kodi ya gari ni kubwa kuliko Bei ya kununulia yote hiyo sababu Kama hizo

Mlaaniwe kabisa shame to all maCCM's!
 
Sas kilichokufanya ukae kweny kochi hivy hivyo ni nini au mikoan maji pia ni shida ?
 
Nahisi jamaa kalewa ...hakuna uhusiano na Barbara zetu
 
Chadema wametuchelewesha sana, hakuna hata kuoga ww nenda hata kazini hvy hvy
 
Mbona Kama matope amepakwa..... Angalia vizuri.

Kuna kipindi miaka ya nyuma nikienda na mzee shambani Kabuki. Nilikuwa ndio nimemaliza f4. Mzee alikuwa na Nissan double cabin kipindi hicho. Kulikua na mvua kubwa, kutoka shambani mbele kidogo tu gari ikakwama.

Sasa kule kabuku Kuna kambi ya jeshi, gari imekwama katikati ya barabara, wakatokea wanajeshi wanafunzi Lori zima na maafande wao nadhani walikuwa wanaelekea kabuku mjini.

Kuona gari imekwama wakashuka wakamwambia mzee ingia ndani ya gari, na Mimi nilivyo bwege nikaingia wakaisukuma ile gari mpaka sehemu salama. Mzee alivyo mstaarabu akapaki akashuka awashukuru, lilikuwa kosa kubwa, wale jamaa walinibeba Hadi kwenye kidimbwi Cha maji machafu wakaniogesha na matope mwili mzima. Dah sitakaa nisahau.

Nilienda kuoga kwenye transit motel pale segera.
 
Mbona hujasema ni mkoa gani hapo Kenya inapopatikana hiyo barabara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…