Sasa BAKITA wana sheria/kanuni inayowapa mamlaka ya kumchukulia mtu hatua za kisheria kwa kosa la kubuni misamiati bila kurasimishwa na BAKITA au kubadili maana ya misamiati iliyopo.
Kuna uchafuzi mwingi wa lugha adhimu ya Kiswahili. Mifano hii hapa:-
1. Kalamu - Peni/pen.
2. Butcher. Kiswahili chake ni nini? Je, ukiandika kwa Kiswahili Bucha nyama haitanunulika? Au watu watakuja kuulizia mkaa badala ya nyama? Je, butcher/butchery ni mchinjaji? Machinjio? Duka la kuuzia nyama? Tuko sahihi tukisema Meat Shop badala ya butcher? Je, meat shop ni Kiswahili?
3. Markiti toka Market badala ya soko.
4. Skuli toka School badala ya shule.
5. Namba 4 na 5 hazijatokana na kibantu zimetokana na English ambayo siyo kibantu.
BAKITA inachelewesha Kiswahili kusambaa. Nchi zilizohitaji Walimu wa Kiswahili zinatumia vitabu vya Kiswahili vya Kiada na Ziada to DR Congo na Kenya, Tz imepigwa bao.
Watz, wajinga ndiyo waliwao.
Siku Kenya wakisema Kiswahili ni chao tunaanza kuwakatalia kama tunavyowakatalia mlima Kilimanjaro. Hata wakati mlima unapigiwa kura duniani, kura za Tz zilikuwa chache kuliko za Kenya.
Lugha zote zinakwenda kwa misamiati inayobuniwa na watu.
Kila mwaka utasikia Oxford wameingiza maneno mapya kwenye kamusi yao ya Kiingereza, maneno yatambulike rasmi, kwa sababu inaonekana yanatumika sana.
Kuna waingereza mpaka leo hawapendi kutumia maneno kama "boss", kwa sababu zamani hili neno lilikuwa slang, leo linatambulika kama Kiingereza rasmi. Sasa wale wahafidhina hawapendi maneno kama haya.
Wataalam walijaribu kutunga lugha zao zinazotungwa na mabaraza, kama Esperanto.
Zimekufa kutokana na kutokuwa na nguvu ya umma.
Kama neno "Mzungu" linatudhalikisha, watu wapewe elimu, wajue, watalikataa wenyewe.
Kama ni sehemu ya utamaduni wetu tu, watu wataamua wenyewe.
Hatuhitaji kushikiwa kiboko na BAKITA. Watu, wakishakuwa nanm elimu, ndio wataielekeza BAKITA.
Kuna mtu anakijua na kukipenda Kiswahili kuliko Rais Ali Hassan Mwinyi hapa?
Mzee Mwinyi kaandika kitabu "Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu". Kitabu kina maneno mengi tu ya mtaani, hususan yaliyotumika katika uongozi wake. Kwa sababu Mwinyi, gwiji la Kiswahili, anajua kwamba maneno yale yanawakilisha moja kwa moja hata hisia ya wakati ule tu, na mengi yalianza kama maneno ya mtaani (slang), lakini yakaja kukubalika kwenye Kiswahili rasmi.
Lugha inakua, na inakuzwa na watu, si mabaraza.