Bagonza Funguka Uliposimamia!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Jambo Member's @JF.
Jambo Moderators@JF.

Niende kwenye Mada yangu moja kwa moja.

Jana viongozi wa madhehebu ya kidini walifanya kikao na Mh Rais wa JMT[emoji1241].

Ombi mojawapo kubwa ilikuwa kuomba msamaha wa kodi kwa vifaa na misaada wanayoipokea kutoka nje ya nchi.

Kulikuwa na mambo mengi yaliyoongelewa ikiwemo pia kuombewa msamaha kwa Mwenyekiti wa chadema, Bwana Freeman Aikaeli Mbowe.

Leo hii 03/03/2022,kupitia kituo cha redio ya Ujerumani, DW-SWAHILI tumemsikia askofu Dk,Benson Bagonza,wa kanisa la Kiinjili la kilutheri jimbo la Karagwe.

Akiongea kupitia redio hiyo amesema wao walikwenda Ikulu kushauri na sio kuomba.
Pia ameendelea kusema Rais anao Uhuru wa kukubali ushauri wao au kuukataa.

Ila anachomekea kwamba kwa Maoni yake Rais anapaswa kutumia Busara yake kwa mambo ambayo yanawakasirisha watu wengi.

Na hivyo yeye anasema anashauri,Rais aingilie muhimili wa mahakama na kumsamehe MBOWE juu ya mashtaka yanayomkabili.

Nimetafakari sana maneno yake na nikakumbuka jambo.
Kwenye ule mkutano wa jana kulikuwa na Uwakilishi mdogo kutoka madhehebu ya RomanCatholic nchini.

Tofauti na tulivyozoea wakiwakilishwa na Maaskofu wao.
Kwa jana waliwakilishwa na Padri mmoja tu.
hakuwepo askofu yeyote kulingana na uzito wa kikao kile,jambo ambalo sio kawaida yao.

Huenda inaweza kuwa inatokana na uzito wa siku ya jana.
Kwani ilikuwa ni Jumatano ya Majivu na hivyo Maaskofu husika kuwa na shughuli nyeti kwenye Mimbari ya kanisani.
Wakitimiza majukumu yao Rasmi.

Ila kwa KKT,pamoja na Askofu Bagonza Kutoka Karagwe,alikuwepo pia Askofu mkuu wa kanisa hilo kutoka Moshi Askofu mkuu
Gideon Shoo.

Mimi ningemuomba Bagonza aachane na Mambo ya siasa zaidi au ajitokeze wazi kama yule mwingine Askofu @Bandekile Mwamakula.

Chadema walikwisha sema hawataki neno msamaha bali kuachiwa.

Bagonza huwa anajulikana rasmi kwa mahaba yake ya wazi kwa Chadema hususan Makamu mwenyekiti wa Chadema mh, Lissu.
Picha zinaongea zenyewe
[emoji116]
View attachment 2137358View attachment 2137359View attachment 2137361
 
Nitakuwa naingilia Uhuru wa akili yangu kama nitailazimisha kuamini kuwa una akili.
Yaani DPP kuondoa kesi mahakamani kwa Nolle proseque ni kuingilia Uhuru wa mahakama? Au unadhani hatukusikia alichoongea Bagonza na DW? Mbona kasema wazi kesi iliyopo mahakamani ni Jamhuri Vs Mbowe & Others, na Mkuu wa hiyo Jamhuri ni Rais. Wapi hujaelewa tukueleweshe?
 
Tupe kifungu cha katiba kinachoruhusu Rais kufuta kes!
 
Msikie askofu Benson Bangoza live akihojiwa na DW :

Jamhuri vs Mbowe na wenzie 3, askofu Bangoza kwa kifupi anamjibu mtangazaji swali lake kuhusu kuingilia mhimili kwa kuuliza Jamhuri ktk kesi namba 16/ 2021 ambayo ni mlalamikaji ni nani kama siyo serikali ? mwisho wa kumnukuu askofu Bagonza.

Sasa sisi watu wa kijiweni hapa JF tunajiuliza Je mlalamikaji kwa busara hawezi kujitoa ktk kesi ili kuiondolea mzigo Mahakama ?

 
[emoji419]Kwa hiyo Rais anaposema tuiache mahakama ifanye kazi yake huwa yuko Wrong?

[emoji871]Lakini si ni nyinyi hao hao mliomtukana na kumkejeli Zitto Zuberi Kabwe kwa kutoa Ombi kama hili hili hapo awali.

[emoji871]Mara kadhaa kupitia Maria Sarungi Space,tumewasikia viongozi waandamizi wa Chadema kina Heche,Lema wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wao Lissu wakipinga Mbowe kupewa Msamaha.

[emoji871]Sasa inakuwaje mnataka kula Matapishi yenu kupitia Kwa Shoo na Bagonza?

[emoji419]Au ni baada ya kuona sasa Maji ya Shingo.
View attachment 2137436
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…