Ina itwa Bachelor of Science in Electronic Sciences and Communications.
Ni kozi pana kama jina lake lilivyo. Ni pana kuliko hiyo ya telecoms ama kozi za computer sciences.
Ina husu sayansi ya umeme mdogo (electronics) kama vile mifumo ya computer, simu, tv, radio, mashine za kielektronic viwandani, ktk afya na nyanja nyingine. Na mifumo ya mawasiliano kama vile ya computer, mawasiliano ya simu, radio, tv, vifaa vya uchunguzi kama vile wa afya, hali ya hewa na kadharika.
Soko lake ni ktk viwanda, idara Zote zenye mashine za kielectronic, idara za computer, makampuni ya simu, na utangazaji -radio, tv, majeshi n.k.
Miaka ya nyuma kozi hii ndiyo ilikuwa ina chukua wanafunzi wachache wenye ufaulu wa juu zaidi wa PCM, na ilikuwa pale UDSM peke yake.
Ni kozi nzuri.