Huko Babati mikoani Manyara juzi kuliibuka taharuki baada ya mtoto wa darasa la tano anayejulikana kama Mathayo Ezekiel kuamua kujinyonga hadi kufa na kumfuata mwanafunzi mwenzie ambaye naye alijinyonga mwezi januari mwaka huu.wanafunzi hawa wanaketi dawati moja katika shule wanayosoma. Hawa wote ni wanafunzi wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 tu.
Si hayo tu kwani nchi nzima sasa kuna vifo vya ajabu ajabu kwa watoto na vijana wadogo kabisa huku hadi wengine wakiamua kujipiga risasi! Huko njombe wanachinjwa. Simiyu nako si shwari. Huko Bunju wanahukumiwa kwenda jela maisha. Kule Kinondoni na Kigamboni wanauawa kwa risasi baada ya walengwa kukoswa. Nini kinaikumba Tanzania awamu hii? Ni laana ya mtoto yule?
Ndugu Sam, matokeo kama haya yameongezeka ulimwenguni, na sio special kwa TZ tuu. Ulimwengu wa sasa kuna mambo mengi yanachangia, ukianzia kwa watoto wa siku jizi wako exposed sana kwa mengi.
1. Wazazi wengi siku hizi hawako responsible. Hawatumii wakati mzuri na familia au watoto wao, ndoa kuvunjika kirahisi. Wazazi kugombana mbele ya watoto bila kujali madhara.
2. Information nyingi sana, na watoto hupenda kuigizana.
3. Walimu siku hizi tena haswa nchi zetu za Africa, wengi hawachukui jukumu lao, la kuwajulia hali za wanafunzi. Na pia mafao ya walimu kutoongezeka, na masingara yao kutoboreshwa na serekali.
Kwa hii issue ya mtoto wa pili kujinyonga, hapo kuna udhaifu mkubwa wa idara ya shule husika , Polisi wa area hiyo na viongozi wa babati. Watoto wa hilo darasa ama shule , ingefanywa uchunguzi wa effect ya yule marehu wa kwanza alipojinyonga, na wakajua, jee tukio hilo limewaletea wenzake physiological effect gani, pengine wangegundua huyu wa pili alikuwa amedhurika.
Society pia tuna mapungufu yetu
Sent using
Jamii Forums mobile app