Babati: Mikasa ya wanafunzi wawili waliokuwa wanakaa dawati moja kujinyonga vifo vikipishana mwezi tu

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,635
2,000
Huko Babati mikoani Manyara juzi kuliibuka taharuki baada ya mtoto wa darasa la tano anayejulikana kama Mathayo Ezekiel kuamua kujinyonga hadi kufa na kumfuata mwanafunzi mwenzie ambaye naye alijinyonga mwezi Januari mwaka huu.Wanafunzi hawa wanaketi dawati moja katika shule wanayosoma. Hawa wote ni wanafunzi wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 tu.

Si hayo tu kwani nchi nzima sasa kuna vifo vya ajabu ajabu kwa watoto na vijana wadogo kabisa huku hadi wengine wakiamua kujipiga risasi! Huko njombe wanachinjwa. Simiyu nako si shwari.

Huko Bunju wanahukumiwa kwenda jela maisha. Kule Kinondoni na Kigamboni wanauawa kwa risasi baada ya walengwa kukoswa. Nini kinaikumba Tanzania awamu hii? Ni laana ya mtoto yule?
 
kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,647
2,000
Hapa mwisho umechapia umbea vinginevyo nenda polisi karipoti hilo tukio la mtu kupigwa risasi. Huyo aliyefungwa maisha kahukumiwa na mahakama kwa makosa yake na havina uhusiano wowote na matukio uliyotangulia kuyataja. Kuna kitu unatafuta tu wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Golobeja

Member
Aug 20, 2017
90
125
Huko Babati mikoani Manyara juzi kuliibuka taharuki baada ya mtoto wa darasa la tano anayejulikana kama Mathayo Ezekiel kuamua kujinyonga hadi kufa na kumfuata mwanafunzi mwenzie ambaye naye alijinyonga mwezi januari mwaka huu.wanafunzi hawa wanaketi dawati moja katika shule wanayosoma. Hawa wote ni wanafunzi wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 tu.

Si hayo tu kwani nchi nzima sasa kuna vifo vya ajabu ajabu kwa watoto na vijana wadogo kabisa huku hadi wengine wakiamua kujipiga risasi! Huko njombe wanachinjwa. Simiyu nako si shwari. Huko Bunju wanahukumiwa kwenda jela maisha. Kule Kinondoni na Kigamboni wanauawa kwa risasi baada ya walengwa kukoswa. Nini kinaikumba Tanzania awamu hii? Ni laana ya mtoto yule?
Bundi alilia
 
FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
kama taifa tukae na kumuomba Mungu atuepushie mbali maana siku ghadhabu yake ikiwa kuu juu ya uso wa nchi yetu , hakuna atayeweza kunywa mvinyo wa kikombe hiko.
 
Hawachi

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
12,120
2,000
kama taifa tukae na kumuomba Mungu atuepushie mbali maana siku ghadhabu yake ikiwa kuu juu ya uso wa nchi yetu , hakuna atayeweza kunywa mvinyo wa kikombe hiko.
Hii Nchi hata kuiombea unapata laana.
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,272
2,000
Huko Babati mikoani Manyara juzi kuliibuka taharuki baada ya mtoto wa darasa la tano anayejulikana kama Mathayo Ezekiel kuamua kujinyonga hadi kufa na kumfuata mwanafunzi mwenzie ambaye naye alijinyonga mwezi januari mwaka huu.wanafunzi hawa wanaketi dawati moja katika shule wanayosoma. Hawa wote ni wanafunzi wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 tu.

Si hayo tu kwani nchi nzima sasa kuna vifo vya ajabu ajabu kwa watoto na vijana wadogo kabisa huku hadi wengine wakiamua kujipiga risasi! Huko njombe wanachinjwa. Simiyu nako si shwari. Huko Bunju wanahukumiwa kwenda jela maisha. Kule Kinondoni na Kigamboni wanauawa kwa risasi baada ya walengwa kukoswa. Nini kinaikumba Tanzania awamu hii? Ni laana ya mtoto yule?
Ndugu Sam, matokeo kama haya yameongezeka ulimwenguni, na sio special kwa TZ tuu. Ulimwengu wa sasa kuna mambo mengi yanachangia, ukianzia kwa watoto wa siku jizi wako exposed sana kwa mengi.

1. Wazazi wengi siku hizi hawako responsible. Hawatumii wakati mzuri na familia au watoto wao, ndoa kuvunjika kirahisi. Wazazi kugombana mbele ya watoto bila kujali madhara.
2. Information nyingi sana, na watoto hupenda kuigizana.
3. Walimu siku hizi tena haswa nchi zetu za Africa, wengi hawachukui jukumu lao, la kuwajulia hali za wanafunzi. Na pia mafao ya walimu kutoongezeka, na masingara yao kutoboreshwa na serekali.

Kwa hii issue ya mtoto wa pili kujinyonga, hapo kuna udhaifu mkubwa wa idara ya shule husika , Polisi wa area hiyo na viongozi wa babati. Watoto wa hilo darasa ama shule , ingefanywa uchunguzi wa effect ya yule marehu wa kwanza alipojinyonga, na wakajua, jee tukio hilo limewaletea wenzake physiological effect gani, pengine wangegundua huyu wa pili alikuwa amedhurika.

Society pia tuna mapungufu yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,536
2,000
Naskia yule laprofeseri anatanua tu mtaani bila wasiwasi na msibani kahudhuria tena kagharamia huo msiba.
Mke alkua kubangua korosho yy kabaki huru kula utamu. Katia na mimba kabisa. Issue ikaja kwny kutoa dem kagoma..mtto hataki. Wife na anazngua balaa simu na mikwara havikomi. Basi, baada ya hapo...,
 
Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
16,026
2,000
Maovu ya Tanzania na viongozi wake yamefika mbinguni .

Taifa halieleweki.kila kukicha watu wanajitenga na Mungu. Wazee na wazazi hawajielewi...

Sasa kama wazee nawazaz hawajielewi...unategemea tutaepuka kizazi cha kamari nakubet???
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom