G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,874
Huko Babati mikoani Manyara juzi kuliibuka taharuki baada ya mtoto wa darasa la tano anayejulikana kama Mathayo Ezekiel kuamua kujinyonga hadi kufa na kumfuata mwanafunzi mwenzie ambaye naye alijinyonga mwezi Januari mwaka huu.Wanafunzi hawa wanaketi dawati moja katika shule wanayosoma. Hawa wote ni wanafunzi wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 tu.
Si hayo tu kwani nchi nzima sasa kuna vifo vya ajabu ajabu kwa watoto na vijana wadogo kabisa huku hadi wengine wakiamua kujipiga risasi! Huko njombe wanachinjwa. Simiyu nako si shwari.
Huko Bunju wanahukumiwa kwenda jela maisha. Kule Kinondoni na Kigamboni wanauawa kwa risasi baada ya walengwa kukoswa. Nini kinaikumba Tanzania awamu hii? Ni laana ya mtoto yule?