Shikamoo Mzee Said. Hongera kwa uandishi wako kwa njia ya vitabu na makala.Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.
Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.
Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.
Mkoloni alikutawala kwasababu ulikua muislamu au mwafrika ..waarabu walichukua watumwa hapa tanzania kwasababu walikua wakristu au waafrika.
Hii inaleta mantiki na inaonesha kweli unafuatilia kwa karibu. Kuna sababu ya kulalamika...lakini bado pia acknowledge some of the factors kwa baadhi ya positionsKong...
Uadilifu II
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:
Mawaziri na Manaibu: 30.
Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.
Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.
Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.
Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.
Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.
Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.
Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.
Wakurugenzi mbalimbali: 249.
Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.
Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.
Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.
Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.
Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33
Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.
Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.
Jumla Kuu ya Uteuzi:
Waislamu asilimia 20%.
Wakristo asilimia 80%.
Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.
GE2020 - Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania
Bismillahir Rahmanir Rahiim SHURA YA MAIMAMU TANZANIA WARAKA [MWONGOZO] UCHAGUZI MKUU WA TAIFA OKTOBA 2020 TANZANIA Umetolewa leo Tarehe 09. 07. 2020. UTANGULIZI Ugonjwa wa Korona – COVID-19 Sote Tunafahamu kuwa nchini mwetu na Dunia kwa ujumla kumekuwepo na taharuki kubwa ya Ugonjwa wa...www.jamiiforums.com
Hii ndio maana wazee kama hawa nyerere aliwapiga chini na nina furahi mtu kama huyu anapima watanzania kwa jicho la dini hafai katika jamiiHii inaleta mantiki na inaonesha kweli unafuatilia kwa karibu. Kuna sababu ya kulalamika...lakini bado pia acknowledge some of the factors kwa baadhi ya positions
Ada...Nauliza swali moja tu. Nyerere alipokewa na wazee wa dar au waislamu.?
Ed...Hii ndio maana wazee kama hawa nyerere aliwapiga chini na nina furahi mtu kama huyu anapima watanzania kwa jicho la dini hafai katika jamii
Soine,Shikamoo Mzee Said. Hongera kwa uandishi wako kwa njia ya vitabu na makala.
Hongera pia kwa kutetea usawa katika jamii.
Mzee Said nimekuwa mfanyakazi wa umma sehemu mbalimbali, kiukweli sijawahi ona sehemu ambayo ilifanyika makusudi na viongozi au sekretariati ya ajira kutoajiri mtu kwa sababu ya dini yake. Kikubwa ni sifa ya mtu wala sio dini. Ungesema kabila na ukanda hapo tungekuelewa kidogo maana kuna baadhi ya taasisi huko nyuma (sio enzi hizi za sekretariati ya ajira) zilijaa watu wa kabila au kanda fulani.
Udini kidogo umeanza kurise kuanzia 2000s tena kwa baadhi ya taasisi.
Huko nyuma ni kweli kulikuwa na gap kubwa kati ya mkristo na muislamu (sababu kubwa ilikuwa elimu, kuna upande uliwekeza zaidi elimu ya dini kuliko elimu dunia), ila kwa sasa wengi wa vijana na watoto wa kitanzania wamesoma bila kujali dini wala kabila....hata jamii za waokota matunda na mizizi pamoja na wafugaji wako wengi kwenye mfumo wa elimu na ajira.
Hivyo, Mzee wangu tambua hilo gap la elimu lilivyokuwa huko nyuma ukizingatia taasisi nyingi za elimu zilikuwa chini ya dini fulani.
mzee heshima yako, je watanzania kwako ni dini au mwafrika aliyezaliwa ndani ya tanzania.Ed...
Unaona sawa kuwa na 20:80?
Hongera sana.Kinyungu,
Sikupenda niliseme hili lakini nitalisema kukutoa shaka.
Mwaka wa 2011 nilialikwa University of Iowa, Marekani.
Likaja swali kama hili lako katika mhadhara niliofanya pale.
Wao wakaja na takwimu za CIA kuhusu "religious distribution," Tanzania na kueleza kuwa madaraka yamehodhiwa kwa wingi uliokuwapo.
Jibu langu lilikuwa swali kwa hadhira yangu ambayo yote ni hao watupu ukumbi mzima na wote ni maprofesa wa historia.
Nikawaomba wanipe mfano wa nchi moja duniani ambayo imevamiwa na wakoloni kutoka nje na waliosimama kunyanyua silaha na kupigana na wavamizi wakawa ni wale wachache.
Hapa nikatoa mfano wa Vita Vya Maji Maji.
Kwa bahati katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin ambae ameandika kitabu cha Maji Maji.
Nikatoa mfano mwengine nikauliza harakati za Waafrika kujitambua na kudai uhuru zilipoanza Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele kudai nchi yao?
Nikawafanyia rejea katika kitabu cha Abdul Sykes ambacho wao wanakifahamu na wanakisomesha kama rejea katika historia ya Afrika.
Nikauliza historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele?
Je ni hawa wachache?
Nikawaomba watoe mfano wa nchi moja tu duniani ambako wachache walisimama kuikomboa nchi yao.
Ukumbi ulikuwa kimya.
Hapakuwa na jibu.
Ukweli ni kuwa siku zote wale wengi ndiyo wanaokuwa na nguvu ya kupambana na adui na wengine huwa nyuma kuongeza nguvu.
Picha hiyo niko darasani nasomesha University of Iowa kushoto ni Prof. James Giblin.
View attachment 2098290
Huenda kweli sijui kwa sababu sijawahi kuwaza wala kuona hilo. Kwa sababu najua ajira ni kwa ajili ya woteSoine,
Hujui.
Na kama hujui ndiyo hujui.
Utasema kile ukijuacho.
Mimi najua na naeleza nikijuacho.
Hakuna tatizo.
Key...Unajuaje kama mimi sipo kwenye 0% ya representation..., Unajua Watanzania wote sio Wakristu au Waislamu..., kuna Traditional African Religions na wengine ni Unaffiliated...
Kwahio na mimi nianze kudai representation sababu ya Imani yangu na sio Weledi wangu ? Nadhani hii vita tungeipigana wote kuondoa uduni wa kila Mtanzania / Mtanganyika na sio kugawana umasikini (as I see it watanzania wengi ni duni no matter their beliefs)
Historia yako unataka ianzie lini na wapi ? Nikikwambia kwamba wazee wetu waliteseka na hata huo udhalimu kuja baada ya hizi dini kuja na Merikebu takuwa ninakosea ?Key...
Majibu si mepesi kama unavyodhania.
Wazee wetu wamepigania uhuru wa nchi hii kuondoa udhalili.
Soma historia ya Waislam katika Maji Maji hadi siasa za TANU unakuja na habari za Wapagani.
Kuna Wapagani waliokuwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Au una picha hata kipande ya wachungaji wamepiga na Nyerere wakati wa ukombozi wa nchi hii?
Huna unachokijua katika tatizo hili.
Wanaostahili kujibu wako kimya.
Jitulize soma historia hii kwanza uielewe.
Belgian Congo slave trade ni tofauti na Transatlantic slave trade?Key...
Ikiwa unataka tujadili historia ya utumwa vyema niko tayari.
Tuanze na Transatlantic Slave Trade.
Kisha tuingie Belgian Congo Slave Trade.
Karibu.
Computer,Belgian Congo slave trade ni tofauti na Transatlantic slave trade?