Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Haya ndio yanawaumiza? Mna shida mahali nyie watu!! Vp Zanzibar ambako hakuna kiongozi mkristo hata mmoja?
 
Mzee inaoneasha wazi una msongo wa mawazo ambao aidha umesababishwa na malezi au makuzi enzi ya utoto/ujana wako.ekja na
Pole sana...M/Mungu akufanyie wepesi!
Ngoru...
Hapa barzani kuna kila aina ya mambo.
Kuna wanaoniita ''mchochezi,'' ''kanjanja,'' ''mdini,'' ''siasa kali,'' nk. nk.

Sasa umekuja na ''msongo wa mawazo.''
Katika maisha yangu sijagusa aina yoyote ya ulevi.

Ningekuwa na msongo wa mawazo nisingeweza kufanya mengi niliyofanya udogoni na katika ujana wangu.

Hili la malezi yangu nakupa kazi nichunguze katika maandishi yangu na shughuli zangu utanijua.

Huwezi kuwa na msongo wa mawazo ukawa na uwezo wa kutuliza ubongo wa kujadiliana na watu kila siku kila wakati.

Nadhani unajua kuwa mimi hapa nasomesha.
Hiyo picha hapo chini ni leo asubuhi:


Majadiliano na Hemed Lubumba, ''Safina ya Maarifa,'' IBN TV.
 
Mag...
Sykes Mbuwane kaingia Tanganyika akiwa Muislam na alikuwa na nduguye kipofu wamekuja pamoja anaitwa Ali Katini.

Ally Sykes alipozaliwa alipewa jina la Ally ambae ni babu yake.
Ramadhani Mashado Plantan kaingia Tangnayika 1905 akiwa na umri wa miaka 5 akiwa Muislam.

Ally Sykes alikwenda kijijini kwao Kwalikunyi Msumbiji alipotoka babu yake na kawakuta ndugu zake Waislam.

Hii ilikuwa 1952.
Ukiwa mlowezi ni kosa kuandikwa historia yao?

Sasa historia ya Kleist Sykes ipo katika Dictionary of Afrian Biography na mwandishi ni Mohamed Said.

Historia ya Abdul Sykes kipo kitabu kizima (1998) na tuaingia sasa toleo la 5.
Tuifute historia hii kwa kuwa ni mjukuu wa mlowezi?

Tuzifute kadi za TANU na 2 na 3 ya Ally na Abdul Sykes?
(Kleist Sykes yupo ndani ya Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam:

(Daisy Sykes Buruku, ''The Townsman: Kleist Sykesí, katika Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, uk. 95-114. Angalia A.D. Sykes ''The Life of Kleist Sykes,'' University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).

Lakini ukitaka kustarehe fika Library of Congress, Washington angalia Sykes au Google uone nini kimehifadhiwa.

Tunaweza tukafuta historia hii yote?

Njia nyepesi ni nanyi mkaandika historia ambayo itaweza kupambana na histori hii ya wazee wangu.

 
Sykes Mbunyewane alikuwa anaswali masjid gani huko Uzuluni kwao? Huu ni uwongo. Weka uthibitisho mzee.
 
Hee kumbe macomedian wamekuwa ni madaktari?
Mzee Mo,nakushauri kama Dr...kwa umri uliofikia si vyema kubeba vitu vingi akilini,hasa vile vinavyokukwaza!
Wise...
Nina vitu vingi akilini watu wengi wananiambia hivyo.
Lakini katika hivi vitu ni elimu na maarifa.

Katika hivi vitu nilivyobeba sina kitu chochote kinachonikwaza.
 
Sykes Mbunyewane alikuwa anaswali masjid gani huko Uzuluni kwao? Huu ni uwongo. Weka uthibitisho mzee.
Schmidt,
Yote hayo ya nini ndugu yangu kama ni uongo basi acha ubakie uongo kwangu.
 
Schmidt,
Yote hayo ya nini ndugu yangu kama ni uongo basi acha ubakie uongo kwangu.
Wewe si Mwanahistoria? Jee, umewahi kukanyaga huko Uzuluni ukauona msikiti aliokuwa akiswali Babu yako, na kuchunguza mazingira ya Uislamu wake huko?
 
ksk,
Kwa kweli umenistua sana na taarifa hii.
Unakusudia Chief Michael Lukumbuzya?

Naweza kupata hizo picha?

Hebu soma hii:

''Katika mazungumzo kama haya ndipo siku moja Mama Daisy akanihadithia habari za Chief Luumbuzya.

Anasema walitoka Dar es Salaam yeye mumewe kwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.

Walipanda meli Mwanza pamoja na Chief Lukumbuzya kuelekea Nansio.

Lukumbuzya alikuwa anatokea Makerere Uganda alipokuwa anasoma anarudi nyumbani likizo.

Abdul Sykes na Michael Lukumbuzya hawakuwa wanajuana.

Hamza Mwapachu alikuwa amekusanya wananchi na kikundi cha ngoma kuja kumpokea bandarini Nansio President wa TAA Abdulwahid Sykes.

Lukumbuzya alishangazwa kukuta sherehe bandarini akifanyiwa mtu ambae yeye hakuwa anamjua na akiuliza anaambiwa mgeni ni mgeni kutoka Dar es Salaam.

Lukumbuzya alipigwa na butwaa kuona mapokezi ya watu wake wa Ukerewe wakiwa katika nderemo wakati yeye chief hakuna hata mtu alikuwa anajua kuwa yumo katika meli ile ile.

Baadae Hamza Mwapachu alimfahamisha yule mgeni waliokuja kumpokea pale alikuwa nani katika siasa za Tanganyika.''


Chief Michael Lukumbuzya
 
Wewe si Mwanahistoria? Jee, umewahi kukanyaga huko Uzuluni ukauona msikiti aliokuwa akiswali Babu yako, na kuchunguza mazingira ya Uislamu wake huko?
Schmidtt,
Nimefika Mozambique mwaka wa 1990 lakini sikufika Kwa Likunyi kijiji alichotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan miaka ya mwishoni 1800.

Lakini nilikwenda kwenye soko kuu la Maputo kuliangalia na sababu ni kuwa katika historia aliyoandika Kleist Sykes kabla hajafa 1949 alieleza kuwa alijitahidi sana kuwatafuta ndugu zake Mozambique akiandikiana barua na bwana mmoja wa Kingazija jina lake Ali Saleh akimwambia kuwa aende hapo sokoni mjini awaulize akina mama wa Kimanyema waliokuwa wanafanya biashara hapo wanaweza wakawa na taarifa za ndugu zake.

Lakini mwaka wa 1990 inakaribia miaka 100 ni muda mrefu kwa hiyo sikuweza kuona mandhari ya soko kama lilivyokuwa miaka ya 1800.

Eid Haj mwaka huo ilinukuta Maputo na nilisali Eid msikiti mkubwa wa Maputo ulikokuwa katikati ya mji.


Rovuma Hotel Maputo 1990
 
Wewe si Mwanahistoria? Jee, umewahi kukanyaga huko Uzuluni ukauona msikiti aliokuwa akiswali Babu yako, na kuchunguza mazingira ya Uislamu wake huko?

Wewe ulishafika ? Hivi unajua historia ya Hao watu
 
Mzee anawanyosha![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee anawanyosha![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
King...
Usiseme hivyo ndugu yangu.
Mimi nashukuru kuwa nilizaliwa wakati huo na watu hao.

Hii ndiyo imenifanya mimi kuwa sehemu ya historia hiyo na hivyo kujua mengi.
Tuna wajibu wa kuwafundisha wenzetu historia hii.

Haifai kuwananga.
Historia hii imewashtua wengi sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…