Ni ngumu sana kupandisha mishahara wakati mfumuko wa bei haupo undercontrol. Ukipandisha mshahara na bei zina panda exponentially kufidia gepu la ongezeko.
So cha msingi ni kutazamia mbinu za kushusha mfumuko wa bei. Ukiweza hilo automatically mshahara utatosha. Hata kwa mshahara wa 300,000 na nusu watu watafanya maisha issue ni mfumuko wa bei baaaaasi.
Mataifa yetu ya dunia ya tatu bado yanapambana na hili tatizo na linawashinda kwasababu ya kukosa mipango na mikakati ya kiuchumi ya kupambana na soko la uhitaji wa bidhaa na huduma mbali mbali ambazo nyingi hutokea nje.
Unapokuwa na taifa hambalo wanainchi wake 80% ya mahitaji yao hutokea nje ya inchi then tarajia mfumuko mkubwa wa bei kwasababu pesa yote inakwenda nje na wao humu ndani hawana soko linalotegemea bidhaa tokea ndani.