Napenda kuwapa tahadhari juu ya kikundi cha askari wa usalama barabarani wanaopenda kukaa maeneo ya Kimara Kona ama Kimara Bucha. Askari hawa ni wahuni na wanabambikia watu kesi kila mara, na muda mwingine ukibishana nao wanakukariri gari yako na kuchukua number ya leseni yako wanakua wanakuandikia faini ilihali huna kosa wala hujakubaliana na kosa tajwa kama sheria inavyoelekeza.
Wapigeni picha za kutosha muwaweke hapa ili tuwajadili, kuna wengine hawajapata shida kitaa wametoka kwa wazazi, wakapitia kwa mashemeji, wakawa ma askari. Inabidi turekebishe modura assendi yao..
Daa poleni sana..
Mi kuna gari langu lina plate namba za kawaida ila sio langu nila ofisi basi washalijua huwa nikipita wanajishtukia sana maana kuna mmoja nilimbananisha hadi kaomba msamaha
Konda wa daladala moja la Mbezi - Temeke alimwambia dereva wake aliyekata kasimama baada ya kupigwa mkono "twende achana naye alikula elfu tano asubuhi saa hizi anajifanya ametusahau"
Umesema yote rafiki yangu...yani huo ndo mtindo kwa wale wapuuzi! Lile genge lao kwakweli linatakiwa liangaliwe sivyo ni kumtafuta mmoja mmoja jioni anafanyiziwa maana wamekua kero kwakweli
Umesema yote rafiki yangu...yani huo ndo mtindo kwa wale wapuuzi! Lile genge lao kwakweli linatakiwa liangaliwe sivyo ni kumtafuta mmoja mmoja jioni anafanyiziwa maana wamekua kero kwakweli