Asante mlioitabiria Simba kipigo cha 5G

Jeff kacheza soka au kajifunza kuhadithia soka? Wanapoitwa wachambuzi "uchwara" maana yake ndo hii! Bado mmoja kuumbuka.
 
Hawa wanaoongoza mashambulizi ya nje ya uwanja dhidi ya Simba ni wachambuzi wa soka makanjanja wakitumia media kuwakuza wanaowapenda.
Hata kama mnaipenda utopolo lazima ifike mahali muwe na heshima ijapo kidogo.Mnapima uwezo wa Simba kwa kucheza na Dodoma jiji?!!!
Mmeanza lini kushabikia mpira?
Kwa hiyo Barcelona aliyefungwa 8 na Bayern ni dhaifu kuliko All ahly aliyefungwa goli 2 tu?
 
Mungu kweli si Athuman,

Baada ya kusoma comments mbalimbali humu kuelekea mechi ngumu ya Simba dhidi ya AS Vita, nilivunjka moyo mno kiasi cha kula chakula cha jioni na baada ya taarifa ya habari nikazima simu na TV na kukimbilia kitandani.

Saa 4.45 usiku nikachungulia YouTube nikaona bado simba haijafungwa halafu mtangazaji anasema Simba wamejitahidi na kwamba mechi ya mwisho katika uwanja ule muda kama huo Simba walikuwa wamekalia 3-0. Nikaona dharau dhidi ya Simba inaendelezwa kiaina.

Nikazima simu japo usingizi hakuna. Nilichungulia tena dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika nikaona Simba 1 wenyeji wao 0. Nikajikaza kuangalia dakika zilizobaki hadi mwisho.

Nikiwa alone room kwangu niliamka kuwasha TV kana kwamba mechi ndo inaanza, nikaishia kuangalia hapa na pale kwa furaha ya ushindi wa Simba.

Kuna mchambuzi anajita Jeff, alisema kwamba kwa beki ile iliyocheza siku ya mechi kati ya Simba na Dodoma, Simba hawatafika mbali. Ni maoni yake, lakini tosha tu kusema kwamba asante kwa walioitabiria Simba mabaya kwa kuwa Mungu amewajibu utabiri wenu na roho mbaya haijengi hata siku moja. Isitoshe dua la kuku halimpati mwewe.

Simba imeanza hivi, inshallah mwenye Mungu aendelee kuisimamia hata katika mechi ya marudiano.

This is Simba. Not utopolo.
 
Serikali itupe ulinzi mashabilki wa Simba.
Uto wana husda wanaweza kutupiga ngumi uwa ni kawaida yao.
 
Mkuu nilifanya hivi kulinda afya. Yale yanayomkuta Manara hadi anapoteza network ndiyo hata mimi hunisibu. Simba au Taifa stars wakicheza huwa ninatetemeka na mwili hushikwa ubaridi hata kama jua linawaka.

We acha tu.
Taifa stars? U can't be serious
 
Mkuu nilifanya hivi kulinda afya. Yale yanayomkuta Manara hadi anapoteza network ndiyo hata mimi hunisibu. Simba au Taifa stars wakicheza huwa ninatetemeka na mwili hushikwa ubaridi hata kama jua linawaka.

We acha tu.
Mkuu hauko peke yako. Wa kweli watu tunatofautiana. Mimi sina uwezo kabisa wa kutizama mechi live ya Simba. Huwa naangalia tv mechi ya marudio, simba imeshinda, au angalau mitandaoni. Au kama naambiwa simba inaongoza kwa magoli mengi! Ni shiiidaaah!
Kuna shemeji yangu kwa kweli nampongeza. Anaangalia mechi dakika ya kwanza, matangazo ya biashara, uchambuzi, mpaka dakika ya mwisho. Naona ana uwezo wa kujichora usimba na kwenda uwanjani live, na hataona shida kurudi na marangi yake kama tumepoteza mechi, huku akizomewa na watu wa Yanga. Kwa kweli mimi siwezi kabisaaa. Mbona nitaugua?
 
Tupeane pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…